Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kuondoa Simu Yako kwenye Hali ya Kustaki

Njia nne za kuweza kuondoa simu yoyote kwenye hali ya kustaki
Jinsi ya Kuondoa Simu Yako kwenye Hali ya Kustaki Jinsi ya Kuondoa Simu Yako kwenye Hali ya Kustaki

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanakuwa na tatizo la simu yako kustaki mara kwa mara basi makala hii ni kwa ajili yako. Kama unavyojua, simu nyingi za Android za sasa zinakuja zikiwa zimefungwa moja kwa moja na hauwezi kufunguka simu hiyo kwa namna yoyote.

Jinsi ya Kuondoa Simu Yako kwenye Hali ya Kustaki

Advertisement

Ni kweli kwamba njia rahisi ya kuweza kuondoa simu kwenye hali ya kustaki ni kutoa battery ya simu hiyo na kurudisha, lakini unafanyaje kama simu yako imefungwa moja kwa moja na huwezi kufungua simu hiyo ili kutoa battery..? Majibu ninayo..

Kwanza awali ya yote labda nikwambie kuwa, hatizo hili limenikuta binafsi na katika hali ya kufanya ufumbuzi nikaona sio mbaya nikishiriki na wewe njia ambazo nilitumia kuweza kuondoa simu yangu kwenye hali ya kustaki.

Kumbuka njia hizi mara nyingi zinafanya kazi kwenye simu za aina zote yaani simu za Android pamoja na simu za iPhone au iOS.

Chomeka Chaji

Jinsi ya Kuondoa Simu Yako kwenye Hali ya Kustaki

Kama simu yako imestaki na upo karibu na chaji yake basi unaweza kuchukua hatua ya kwanza na kuchomeka simu yako kwenye chaji ikiwa kwenye umeme. Kisha subiri kidogo na jaribu kuzima simu yako. Njia hii hufanya kazi kwa simu nyingi ambazo unakuta zime staki kwa sababu ya kufungua programu nyingi kwa wakati mmoja.

Jipigie Simu

Jinsi ya Kuondoa Simu Yako kwenye Hali ya Kustaki

Njia nyingine ambayo unaweza kutumia ni kupiga simu kwenye namba ambayo ipo kwenye simu iliyo staki. Mara nyingi njia hii hufanya kazi hasa kama kuna programu uliyo kuwa unatumia ambayo ndio imefanya simu yako kustaki.

Njia hii kufanya kazi kwa sababu kupigiwa simu huwa kuna fanya simu yako isimamishe kazi zote ikiwa pamoja na kusitisha Matumizi yote ya data kwa muda.

Shikilia Kitufe cha Home (Kama Kipo)

Jinsi ya Kuondoa Simu Yako kwenye Hali ya Kustaki

Kama simu yako ni ya muda kidogo, bila shaka inayo kitufe cha home ambacho huwa tofauti na kioo cha simu yako. Bofya kitufe hicho na kishikilie kwa utaratibu kwa muda wa sekunde tano na utaweza kuona simu yako imetoka kwenye hali ya ku-staki.

Njia hii inaweza kufanya kazi kama simu yako inayo kitufe cha kujitegemea hivyo kama kitufe cha home kipo kwenye kioo cha simu yako basi unaweza kujaribu njia inayofuata hapa chini.

Shikilia Vitufe vya Sauti + Kitufe cha Kuzima

Jinsi ya Kuondoa Simu Yako kwenye Hali ya Kustaki

Njia ambayo mara zote imekuwa ikifanya kazi kwenye simu zote ambazo nimesikia zikiwa na tatizo la kustaki ni njia hii ya kubonyeza kwa pamoja vitufe vyote vya sauti (kitufe cha kuongeza na kupunguza sauti) ikiwa pamoja na kitufe cha kuzima na kuwasha simu.

Bofya vitufe vyote kwa pamoja kwa muda wa sekunde tano, au hadi utakapo ona simu yako ikizima na kuwaka kwa mara nyingine. Njia hii ni moja kati ya njia ambayo inafanya kazi kwenye simu nyingi sana hivyo unaweza kujaribu njia hii kama njia zote hapo juu zimeshindikana.

Bila shaka hadi hapo umeweza kuondoa simu yako kwenye hai ya kustaki, kama unataka kujua zaidi unaweza kusoma hapa kujua mambo yanayo changia simu yako kustaki. Pia utaweza kujua mambo ya muhimu ya kufanya ili kuzuia tatizo hili lisiweze kutokea tena mara kwa mara.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use