Tarehe ya Uzinduzi wa Toleo Jipya la Kompyuta ya Apple MacBook Pro

Kama wewe ni mpenzi wa kompyuta kutoka kampuni ya Apple kaa tayari kwa kompyuta mpya inayokuja hivi karibuni
MacBook Pro MacBook Pro

Kampuni maarufu ya teknolojia ya nchini marekani Apple, hivi karibuni imeanza kutuma mialiko kwa watu mbalimbali ili kuudhuria kwenye mkutano wake utakaofanyika tarehe 27 mwezi huu huko nchini marekani.

Japo kuwa Apple haijatangaza mkutano huo ni kwaajili gani lakini tetesi zinasema kuwa mkutano huo unategemewa kuwa kwaajili ya uzinduzi wa toleo jipya la mwaka 2016 la kompyuta aina ya Macbook pro. Tetesi hizo zinasema kuwa hii ni kwasababu Imepita takribani miezi 17 kutoka kampuni ya Apple ilipotoa toleo jipya la kompyuta hiyo ya Macbook pro, lakini toleo la jipya la Macbook ya inch-13 lilitoka tarehe 9 March 2015 wakati toleo jipya la Macbook ya inch-15 lilitoka tarehe 19 May 2015 na kuacha toleo hilo la Macbook pro. Hata hivyo baadae watu walitegemea kuona toleo jipya la kompyuta hiyo kwenye uzinduzi wa uliofanyika september 7 lakini Apple haikufanya hivyo matokeo yake ulifanyika uzinduzi wa simu za iPhone 7 pamoja na iPhone 7 plus.

Advertisement

Hata hivyo watu wamendelea kuhoji kwamba ni lini kampuni hiyo inategemea kutoa toleo hilo jipya la kompyuta hiyo ya MacBook Pro ya mwaka 2016.?, Basi kama wewe ni mpenzi wa Macbook pro basi usikose kuangalia Mkutano huo kwani bila shaka Apple inategemewa kutangaza toleo hilo jipya siku hiyo ya tarehe 27 october mwaka huu huko nchini marekani (Apple Campus) Cupertino. Taarifa kutoka kwenye tovuti ya 9TO5MAC zinasema kuwa huenda Apple wakatoa matoleo mapya kwa kompyuta zake zote za Macbook na sio tu Apple Macbook pro, tayari mkutano huo umesha pewa jina la “Hello Again” hii ikiashiria kurudi tena kwa toleo jipya la Macbook Pro baada ya kimya cha muda mrefu.

Kuhusi sifa za kompyuta hiyo pamoja na kuangalia mkutano huo live endelea kutembelea tovuti ya Tanzania tech kila siku au Unaweza kuendelea kupata habari za teknolojia kwa kujiunga na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter na Instagram bila kusahau Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni kutoka App Store.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use