Kwa muda sasa tumekuwa tukipata maoni mbalimbali kuhusu baadhi ya watu kushindwa kutumia kwa ukamilifu baadhi ya sehemu kwenye app yetu ya Tanzania tech na sasa tumewaletea suluhisho.
Tanzania tech lite ni app mpya ya Tanzania tech ambayo itakuwa inakupa habari na mafunzo mbalimbali ya teknolojia kutoka tovuti ya tanzaniatech.one. App hii inakuja na mabadiliko na wepesi kutumia zaidi kuliko app ya Tanzania Tech ya kawaida.
Mambo yalipo kwenye App ya Tanzania Tech Lite.
- Matangazo yamepunguzwa sana
- Huna haja ya kulogin ili kusoma makala za Tanzania tech
- Utaweza kuchagua kipengele ukipendacho zaidi
- App ipo kwa Kingereza na Kiswahili
- Muonekano rahisi unaofanya kazi kwa asilimia 100.
- Toleo la lite lina MB 9 tu
- Muonekano wa Dark Mode kwa Asilimia 100 na mambo mengine mengi.
Kama wewe ni mmoja wa watu ambao walikua waki lalamika kuwa link za Tanzania tech hazifanyi kazi kwa usahihi basi hakikisha unapakua toleo hili la Tanzania tech lite kwani kupitia hapa utaweza kufurahia na kujifunza teknolojia kwa urahisi zaidi.
Unaweza kuona muonekani wa app hii kwa kuangalia baadhi ya picha hapo chini.
Unaweza kubadilisha lugha kwa kubofya Settings au kubofya mpangilio kama utakuwa umechagua kiswahili.
Makala zipo kwenye mpangilio ule ule ambao unaupenda huku sasa ikiwa ni rahisi zaidi kufungua makala kwa urahisi na haraka.
Chagua makala uziendazo na pata notification ya habari hizo pekee, unaweza kufanya hivyo kwa kubofya sehemu ya alama ya love kisha bofya mpangilio au settings kisha save au hifadhi.
Vipengele vyote vinaonekana mwisho kabisa kwenye menu na unaweza pia kupanga vipengele kulingana na pendekezo lako kwa kubofya sehemu ya mishale upande wa kulia juu.
Sasa utaweza kutoa maoni kwa urahisi kwa kubofya sehemu ya maoni chini ya makala, ni rahisi na haraka sana.
Hayo na mengine yanapatikan kwenye app ya Tanzania tech lite, jaribu sasa kupakua app hii uweze kujaribu yote yaliyopo ndani ya app hii. Usisahau kutoa maoni yako.
Kwa habari zaidi pamoja na makala za teknolojia hakikisha unapakua app hii au toleo la kawaida la Tanzania tech.