Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Suluhisho la Matatizo ya Teknolojia (Tanzania Tech Group)

Pata suluhisho la matatizo yote ya kiteknolojia kupitia Tanzania Tech Group
Suluhisho la Matatizo ya Teknolojia (Tanzania Tech Group) Suluhisho la Matatizo ya Teknolojia (Tanzania Tech Group)

Kwa muda sasa tumekuwa tukipata maswali mengi sana mengi tukishindwa kuyajibu kwa wakati na mengine tumekuwa tukifanikiwa kuwapa majibu. Lakini swali ambalo tumekuwa tukilipata mara kwa mara na mara nyingi jibu lake limekuwa Hapana ni pamoja na swali la “Kunalo Group la Tanzania Tech.?”.

Zipo sababu nyingi sana za kwanini hakuna group la Tanzania tech, sababu hizo nyingi zikiwa zinazunguka kwenye mada ya kushindwa kusimamia group lolote kutokana na watu kuwa na tabia ya kukiuka matakwa au lengo la group husika. Lakini siku ya leo tumeona tujaribu tena.!

Advertisement

Leo Tanzania Tech tunakuletea Tanzania Tech Group, Group hili linapatikana kwanza kupitia mtandao wa Facebook na baadae tutafikiria kulipanua zaidi kwenye sehemu nyingine kama vile kwenye mitandao ya WhatsApp au Telegram.

Suluhisho la Matatizo ya Teknolojia (Tanzania Tech Group)

Kama maelezo ya Group hilo yanavyosema, group hilo ni sehemu ya kupata suluhisho la maswala yote ya teknolojia, kama unalo swali au kuna kitu chochote kinachohusu teknolojia kina kutatiza kwa namna yoyote basi unaweza kuuliza kupitia group hilo.

Group hili sio la Tanzania Tech pekee, bali mtu yoyote mwenye ujuzi wa teknolojia anakaribishwa kusaidia watu wengine muda wowote. Tunatazimia sehemu hiyo kuwa sehemu ya kupata suluhisho la uhakika kwenye maswala ya teknolojia hivyo natumaini tutapata wataalam wengi wa mambo mbalimbali kupitia group hilo.

Kwa sasa unaweza kujiunga na group hilo kwa kuhakikisha unafuata vigezo na masharti, pia hakikisha unajibu maswali machache ya awali kwaajili ya kufahamiana zaidi. Mengine mengi naamini tutaeleweshana kadri muda unavyo kwenda hivyo naomba kuwakaribisha sana.

Jiunge na Tanzania Tech Group Hapa

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use