Sababu za Kuwa na Ongezeko la Huduma za SimBanking

Matumizi ya huduma za fedha kupitia simu yameongezeka Tanzania na Kenya
SimBanking SimBanking

Katika kuhakikisha kuwa huduma za kifedha zinarahisishwa na kuwezeshwa kwa watu wote nchini tanzania na nchi jirani hivi karibuni Tanzania na Kenya zimetajwa kuwa nchi zenye ongezeko kubwa la matumizi ya huduma za kibenki kwa njia ya simu (simbanking) kwa mwaka 2016. Hata hivyo Mafanikio hayo yametokana na ongezeko la watumiaji wa huduma hizo kwa zaidi ya asilimia 40 katika nchi za ukanda huo kwa mujibu wa ripoti ya Shirikisho la Kampuni za Simu (GSMA), imeripoti gazeti la mwananchi

Akizungumza leo Julai 14, juu ya maendeleo hayo, Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom hapa nchini, Sitoyo Lopokoiyit amesema kuwa hatua hiyo inatokana na kuwapo kwa sera zinazohimiza uvumbuzi na uwekezaji, Amesema kuwa huduma za M-pesa zimeongezeka kwa asilimia 20 mwaka huu na kwamba huduma zimeendelea kuboreshwa ili kuendana na mahitaji ya wateja.

Advertisement

Gazeti la mwananchi lime-endelea kuandika kwa kunukuu “Tumezidi kuboresha huduma za kimataifa na kupungiza gharama,hii ni safari kubwa na inahitaji ushirikiano kati ya wadau wa sekta hii,” amesema mkurugenzi huyo wa Biashara wa Vodacom kwa gazeti la mwananchi, Hata hivyo GSMA imeeleza kuwa hadi Desemba 2016, kulikuwa na jumla ya akaunti za simu 277 na jumla ya miamala 43 milioni hufanyika kila siku kwa nchi hizo za Tanzania na kenya. Pengine kampuni ya vodacom wameliona hili ndio sababu kutanua huduma zake kwa kuleta App yake ya M-pesa mwanzoni mwa mwaka huu.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Chanzo : Mwananchi

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use