Kwa mujibu wa ripoti za hivi karibuni kutoka tovuti ya mwananchi, inasemekana kuwa kampuni ya TALA ambayo inajihusisha na utoaji wa mikopo ya haraka kupitia simu za mkononi, imetangaza kusitisha huduma zake kwa hapa nchini Tanzania.
Sehemu ya ripoti hiyo iliyo chapishwa kwenye akaunti ya Tala kwenye mtandao wa kijamii wa facebook inasema kuwa, “Tunakujulisha kuwa kwa sasa TALA haitoi mikopo nchini Tanzania. Tunathamini nafasi ya kukutumikia na tunatamani wateja wetu waaminifu waendelee na mafanikio katika safari yao ya kifedha, “inasomeka taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo.
https://www.facebook.com/talatanzania/photos/a.1434177873562030/2280933362219806/
Akizungumza na Mwananchi kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Facebook, mmoja wa maofisa wa kampuni hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Kelly amesema, “Ndio, hatujatoa mikopo tena nchini Tanzania. Kwa bahati mbaya, kwa sababu za kisheria hatuwezi kusambaza habari nyingine yoyote isipokuwa ile iliyosambazwa kwenye mtandao wa kijamii.”
Kwa sasa bado hakuna ripoti zaidi juu ya hili hivyo hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech tutakupa taarifa zaidi kuhusu hili.
kwann wasitoe sababu