Jinsi ya Kufufua Spika ya Simu Yako Bila Kufungua

Utaweza kufufua spika ya simu yako kwa haraka na urahisi bila kufungua simu yako
Jinsi ya Kufufua Spika ya Simu Yako Bila Kufungua Jinsi ya Kufufua Spika ya Simu Yako Bila Kufungua

Ni wazi kuwa spika ni sehemu ya muhimu sana kwenye smartphone yoyote, hii ni kwa sababu sehemu hii ndio hutumika kusikiliza hivyo bila spika haiwezekani simu yako kufanya kazi anavyotakiwa.

Kuliona hili leo Tanzania tech tunakuletea njia moja ambayo ni bora kuliko zote ambayo itakusaidia kufufua spika ya simu yako bila kufungua au kupeleka kwa fungi. Njia hii imeonekana kufanya kazi hata kwa spika za simu ambazo zimeingia maji au mate, pia hata na vumbi. Basi bila kuendelea kupote muda moja kwa moja twende kwenye njia hii.

Advertisement

Kwa kuanza tembelea tovuti hapo chini, hakikisha unatembelea tovuti hiyo kwa kutumia simu au smartphone ambayo ina tatizo la spika.

Tembelea Tovuti Hapa

Baada ya kufika kwenye tovuti hiyo moja kwa moja bofya kitufe amcho unakiona kilichopo juu mwanzo wa tovuti hiyo.

Jinsi ya Kufufua Spika ya Simu Yako Bila Kufungua

Baada ya hapo moja kwa moja utaweza kusikia sauti ikitoka kwenye spika yako na endelea kusubiria baada ya muda mfupi kisha bofya tena sehemu hiyo kuzima sauti hiyo na jaribu kusikiliza spika zako kama zimefufuka.

Sasa unaweza kujuliza njia hii inafanyaje kazi..? Kama unataka kujua kuhusu jinsi njia hii inavyofanya kazi ni kuwa, sauti inayotolewa na tovuti hii inafanya spika zako zipulize kwa kwenda nje na hivyo kama spika ina maji ama vumbi basi utaweza kuona vumbi likitoka kwenye simu yako.

Jinsi ya Kufufua Spika ya Simu Yako Bila Kufungua

Kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu sauti hiyo inanguvu kiasi cha kuweza kupuliza hata kitu kilichopo nje. Najua unashangaa na pengine huamini lakini njia hii inafanya kazi kwa asilimia 100, jaribu utaniambia.

Kama unataka kujifunza maujanja zaidi unaweza kutembelea Tanzania tech kila siku, pia unaweza kusoma hapa kujua maujanja ya kupiga picha bora za kuweka kwenye mitandao ya kijamii, nauhakika utaipenda hii.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use