Kampuni ya LG ya nchini korea hivi karibuni imetangaza kuleta simu zake mpya pamoja na vifaa vingine ifikapo mapema January 5 mwaka 2017, Kampuni hiyo pia imetangaza leo kuwa sambamba na kutoa simu hizo kampuni hiyo inategemea kutoa speaker yake mpya ya kisasa yenye uwezo wa kufanya kazi uku ikielea hewani.
Speaker hiyo ambayo inakuja na uwezo wa kucheza muziki kwa nyuzi 360, pia inauwezo wa kucheza muziki ikiwa kwanye maji ya kina kifupi cha meter 1 sawa na (feet 3.3) kwa muda wa dakika 30. Kwa mujibu wa LG speaker hiyo ya Bluetooth inauwezo wa kukaa na chaji kwa muda zaidi ya masaa 10 au zaidi.
Vilevile spearker hiyo iliyopewa jina la PJ9 pale inapoisha chaji hutua taratibu ili kuzuia speaker hiyo isianguke chini na kuharibika na pale tu inapofika chini speaker hiyo huanza kuchaji yenyewe moja kwa moja. Speaker hiyo inakuja na muundo kama yai ambapo huwa juu ya speaker nyingine ya woofer kutoka kampuni hiyo hiyo ya LG.
Kampuni ya LG bado haijatangaza bei ya speaker hiyo, lakini inategemea kufanya hayo yote kwenye mkutano wa maonyesho wa CES utako fanyika huko Las Vegas nchini marekani.