Kampuni ya teknolojia ya Sony hivi karibuni kwenye mkutano wa CES 2017 imetangaza na kuzindua TV yake yenye kutumia teknolojia ya OLED, TV hiyo mpya iliyopewa jina la XBR-A1E Bravia 4K OLED TV ni moja kati ya TV za kisasa za mwaka 2017 kutokana na muundo pamoja na uwezo wake.
TV hiyo imetengenezwea kwa kutumia teknolojia ya Dolby Vision HDR ambayo husaidia kufanya TV hiyo kuonyesha picha na sauti angavu hadi kufikia kiwango cha 4K. Kuipa TV hiyo nguvu inayotakiwa wataalamu kutoka Sony wameweka processor ya kisasa ya 4K HDR Processor X1 Extreme ambayo ndio uendesha TV hiyo nzima.
Kingine bora kuhusu TV hii ni kuhusu wembamba wake, TV hii ni moja kati ya TV ambazo ni nyembamba sana kiasi cha kuonekana kama picha ya ukutani ukitegemea kuwa TV hizo zitapatikana kwa ukubwa wa size za inch 65, na inch 77 hivyo na uhakika lazima zitapendezesha sebule yako pindi zitakopotoka, kuhusu bei Sony bado haijaweka wazi kuwa TV hizo zitauzwa kwa bei gani.
Sony Pia wametoa matoleo mapya ya X940E and X930E ambayo sasa yameboreshwa zaidi kwa wembamba na yamewekewa processor mpya pamoja na teknolojia ya Dolby Vision pamoja na kuongezewa uwezo zaidi wa HDR output.
Kama unataka kujua zaidi kuhusu TV hizi mpya kutoka Sony unaweza kutembelea ukurasa maalumu kwenye tovuti ya kampuni ya Sony.