Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Sony Kuleta Game za Kwenye Simu December 7 Mwaka Huu

Kampuni ya sony yatangaza rasmi kuanza kutoa game zake kwenye mifumo ya Android na iOS
sony-game sony-game

Kampuni maarufu ya teknolojia ya Sony hivi karibuni imetangza rasmi tarehe ya kuleta game zake kwenye mfumo wa Android na iOS. Kufuatia tangazo lililotangazwa mwezi April mwaka huu Sony ilikua mbioni kutengeneza sehemu ya kampuni yake (Forward Works) ambayo ndio itakua ikijihusisha na utengenezaji wa game kwaajili ya smartphone (Android na iOS).

Hata hivyo taarifa za kutoka kwa tarehe ya kuanza kwa game hizo ndio kidhibitisho kuwa sehemu ya kampuni hiyo ya Sony sasa imekamilika na iko tayari kutoa game kwaajili ya smartphone. Sony ni moja kati ya kampuni maarufu sana za utengenezaji wa video game ambayo inafuatiwa na kampuni nyingine nyingi kama vile Nintendo ambayo nayo pia hivi karibuni ilianza kujikita zaidi kwenye simu za mkononi kwa kuanza kutoa game ya Smartphone ya Miitomo na badae kufuatia na game maarufu ya Pokemon Go.

Advertisement

Game hizo za smartphone kutoka kampuni ya Sony zitaanza kupatikana kwenye Play Store na App Store mwezi december mwaka huu kwa nchi za japan na baadae kusambaa dunia nzima.

Kama unataka taarifa lini game hizo zitafika Tanzania endelea kutembelea tovuti ya Tanzania tech au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya  Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use