Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Angalia Status za Mtu WhatsApp Bila Mtu Kujua (Kuona)

Fanya maujanja zaidi ya 20 kwa kutumia njia hii bora na rahisi
Angalia Status za Mtu WhatsApp Bila Mtu Kujua (Kuona) Angalia Status za Mtu WhatsApp Bila Mtu Kujua (Kuona)

WhatsApp ni moja kati ya programu inayotumiwa na watu wengi sana siku hizi, programu hii inatumiwa na watu kuliko hata sehemu ya SMS ambayo inakuwa kwenye simu nyingi za Android.

Kuliona hili, leo Tanzania tech nimekuletea njia rahisi ambayo unaweza kutumia programu ya WhatsApp kipekee na kisasa kabisa. Njia hii ni bora kuliko njia nyingine nyingi ambazo unaweza kuwa unazifahamu. Basi bila kupoteza muda twende kwenye makala hii.

Advertisement

Kwa kuanza hakikisha una pakua programu hapo chini, na kabla hujawaza lolote pengine nikushawishi usome makala hii hadi mwisho ili kujua kama hiki ni kitu ambacho unahitaji au laah!.

Download App Hiyo Hapa

Kupitia programu hii utaweza kufanya mambo mbalimbali kupitia programu ya WhatsApp, mambo hayo ni pamoja na.

Kwanza kabisa juu kabisa kwenye app hii utaweza kuangalia Status za watu mbalimbali waliopo kwenye phonebook yako bila wao kujua.

Angalia Status za Mtu WhatsApp Bila Mtu Kujua (Kuona)

Sehemu ya pili kwenye app hii utaweza kutuma meseji kwa mtu yoyote bila kusave namba yake kwenye simu yako. Kupitia sehemu hiyo unachagua code namba za Tanzania kama upo tanzania kusha una andika namba alafu bofya kitufe cha send na utapelekwa kwenye sehemu ya ujumbe kwenye programu ya WhatsApp tayari kutuma meseji.

Angalia Status za Mtu WhatsApp Bila Mtu Kujua (Kuona)

Mbali na hayo, kupitia programu hii pia utaweza kutuma meseji nyingi za WhatsApp kwa watu wengi kwa mara moja. Kama unao wateja wako ambao unataka kuwajulisha kuhusu bidhaa mpya basi sehemu hii ni bora sana, pia kuna video ambayo utaweza kujifunza jinsi ya kutuma meseji kwa urahisi.

Angalia Status za Mtu WhatsApp Bila Mtu Kujua (Kuona)

Mbali na hayo yote kupitia programu hii utaweza kufanya mambo mengine mengi kama kurudisha meseji ambazo mtu ametuma na kufuta kabla wewe hujasoma. Pia Utaweza kupata WhatsApp web kwenye simu yako ambapo unaweza kusoma meseji za simu nyingine kupitia sehemu hiyo.

Pia utaweza kutengeneza Stories kwa urahisi na haraka kwa kutenganisha video ndefu na kuchukua sehemu ambayo unahitaji kwenye video husika.

Mbali na hayo kama unatafuta Status zenye kuleta maana pamoja na maneno mazuri ya kingereza unaweza kupata kuitia app hii, unacho takiwa ni kuchagua category kama vile Love, Sad na moja kwa moja utaletewa maneno yenye maana nzuri na utaweza kucopy na kuweka kwenye WhatsApp yako kwa urahisi na haraka. Pia utaweza kupata Stika nzuri za kushare na watu wako.

Angalia Status za Mtu WhatsApp Bila Mtu Kujua (Kuona)

Pamoja na mambo mengine mengi sana, app hii ni muhimu sana kwa mtu yoyote ambaye anatumia programu ya WhatsApp. Unaweza kujaribu app hii kisha niambie kama umeona programu hii ni msaada kwako.

Basi baada ya hapo utakuwa umeweza kufanya mambo mbalimbali kupitia WhatsApp, kama unataka kujua zaidi unaweza kusoma hapa kujua njia mpya ya kuweka Wallpaper kupitia WhatsApp kwa urahisi na haraka.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use