Kama wewe ni mtumiaji wa simu za Apple zenye mfumo wa iOS 11 basi makala hii ni muhimu sana kwako. Hivi leo kupitia tovuti mbalimbali kumetokea habari kuwa mfumo wa uedeshaji wa iOS 11 umepatikana kuwa na tatizo ambalo baadhi ya simu pale ifikapo saa 12.15am simu hizo kupata tatizo la kimfumo.
Kama ilivyo ripotiwa na tovuti ya iMore pamoja na engineer wa mtandao wa Twitter anaeitwa Yoshimasa Niwa, tatizo hilo linatokana na programu mbalimbali ndani ya simu ambazo hutumia mfumo wa ujumbe mfupi (Notification) ambapo kila inapofika muda huo pale ujumbe unapo ingia basi simu huzima au kupata tatizo la kiufundi kwenye upande wa mfumo wa uendeshaji.
Hata hivyo baada ya watu mbalimbali kupata tatizo hili, Apple imetangaza kuwa sasa toleo la iOS 11 limeboreshwa kwa toleo jingine la iOS 11.2 na ni muhimu sana ku-update simu yako kwenda mfumo huu mpya kwani ndipo itakapo weza kuwezesha tatizo hilo kuondoka.
Apple pia inashauri kuwa ni muhimu kuzima sehemu ya ujumbe kwa kubofya sehemu ya Settings > Notifications alafu zima sehemu ya Notification kwa kuweka OFF, Mara baada ya ku-update unaweza kuwasha sehemu hiyo na kuendelea kutumia simu yako ikiwa salama.
Kwa habari zaidi unaweza kufuata maelezo kupitia tovuti ya Apple Hapa , Hii ni muhimu sana hivyo kama umesoma makala hii ni vyema ukamwambia na mwenzako kuhusu hili ili simu yake isije kuzima.