Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Tengeneza Soko la Mtandaoni Bure Kupitia Blogger (2022)

Pia utaweza kupokea malipo kupitia Tigo Pesa au Mtandao Mwingine
Tengeneza Soko la Mtandaoni Bure Kupitia Blogger (2022) Tengeneza Soko la Mtandaoni Bure Kupitia Blogger (2022)

Ni wazi kuwa hivi karibuni watu wengi sana biashara za mtandaoni zimekuwa na thamani kubwa, hii ni kutokana na janga la COVID-19 ambalo limelazimisha watu wengi duniani kote kujifunza jinsi ya kununua pamoja na kuuza bidhaa mtandaoni.

Kuliona hili hivi leo nimekuletea njia rahisi sana ambayo unaweza kutumia kuanzisha soko la mtandaoni bure kupitia mtandao wa blogger.

Advertisement

Najua inawezekana huamini kama inawezekana, na kwa sababu hiyo unaweza kutembelea tovuti hapo chini kuweza kuona mfano halisi. Unaweza kufanya kama una nunua bidhaa ili kuweza kuona tovuti hii inavyo fanya kazi.

Angalia Mfano Hapa

Tengeneza Soko la Mtandaoni Bure Kupitia Blogger (2022)

Kama umeona tovuti hii ni kitu ambacho unahitaji basi endelea kwa kufuata hatua kwa hatua jinsi ya kutengeneza soko lako la mtandaoni bure kabisa kwa kutumia mtandao wa blogger.

Kwa kuanza moja kwa moja download template kupitia link hapo chini, kisha endelea kwa kufuata hatua hizi kuweza kuweka template hiyo kwenye blogger.

Download Template Hapa

Baada ya kudownload template kwenye kifaa chako (Simu au Kompyuta) moja kwa moja ingia kwenye blogger yako kisha bofya sehemu ya Theme.

Tengeneza Soko la Mtandaoni Bure Kupitia Blogger (2022)

Baada ya hapo moja kwa moja bofya sehemu ya Customize kama inavyo onekana kwenye picha hapo chini. Hakikisha unafuata hatua hizi kama inavyo onekana hapo chini.

Tengeneza Soko la Mtandaoni Bure Kupitia Blogger (2022)

Baada ya hapo bofya Restore ambayo itatokea kwenye Menu hiyo, Menu hiyo ni ya pili kutoka juu.

Tengeneza Soko la Mtandaoni Bure Kupitia Blogger (2022)

Baada ya hapo bofya Upload na endelea kwa kuchagua sehemu ya File kama unatumia simu, au kama unatumia kompyuta moja kwa moja unaweza kuchagua Download na kutafuta file la template hii ulilo pakua kwenye hatua zilizopita.

Tengeneza Soko la Mtandaoni Bure Kupitia Blogger (2022)

Baada ya Ku-upload moja kwa moja utakuwa umefanikisha kupata muonekano kama ulio uona kwenye demo hapo juu. Kitu cha muhimu hakikisha unafuta hatua hizi kwani hii ndio njia ambayo unaweza kupata kila kitu kama inavyoonekana kwenye tovuti ya mfano hapo juu.

Kurasa Muhimu

Baada ya kuweka template yako vizuri sasa nenda kwenye Menu kisha chagua page na tengeneza page zenye kichwa cha habari kama ifuatavyo.

  • Cart
  • Checkout

Ndani ya kurasa hizi usiandike kitu chochote na hakikisha sehemu ya comment imezimwa kwenye kurasa hizi kwa kuchagua menu iliyopo upande kulia kama navyoonekana kwenye picha hapo chini.

Tengeneza Soko la Mtandaoni Bure Kupitia Blogger (2022)

Jinsi ya Kuonyesha Bei

Ndani ya maandishi wakati una andika post unaweza kuandika hivi ili kuonyesha bei ya bidhaa. Mfano kama bei ni shilingi laki tatu basi unaweza kuandika hivi  “price/TZS 300,000” hakikisha alama ya mkato katikati inaonekana pia usiweke alama za funga semi na funga semi.

Yaani itakuwa hivi “price/TZS andika bei kisha weka mkato” au alama ya strike ambayo inapatikana kwenye menu kwa juu kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini.

Tengeneza Soko la Mtandaoni Bure Kupitia Blogger (2022)

Jinsi ya Kuonyesha Size

Kama bidhaa unayotaka kuuza inayo Size mbalimbali unaweza kuonyesha Size kupitia tovuti yako kwa kuandika Size kwa mtindo huu. Kama ilivyo price sasa andika size/GB32.

Tengeneza Soko la Mtandaoni Bure Kupitia Blogger (2022)

Kama bidhaa unayo uza haina size mbalimbali basi unaweza kuachana nayo na usandike kitu chochote kama nilivyo elekeza hapo juu. Kama ukifuata maelezo yote ukurasa wa bidhaa yako utakuwa kama inavyo onekana hapo chini.

Tengeneza Soko la Mtandaoni Bure Kupitia Blogger (2022)

Njia za Kupokea Malipo

Kama nilivyo kwambia awali soko hili linafanya kazi kwa asilimia 100 na unaweza kuruhusu wateja kutuma malipo kutumia njia za keshi unapowafikishia bidhaa na pia unaweza kupokea pesa kwa Tigo pesa na hii ni kwa wale ambao tayari wanao wateja wanao amini soko lako.

Tengeneza Soko la Mtandaoni Bure Kupitia Blogger (2022)

Pele mteja atakapo chagua njia ya malipo na kujaza data zote na kubofya Confirm Order, moja kwa moja anaweza kumalizia kwa kubofya Place Order kisha moja kwa moja wewe utapokea email ya oder ya mteja wako kwenye email ulio jisajili na blogger yako.

Tengeneza Soko la Mtandaoni Bure Kupitia Blogger (2022)

Kama unavyoweza kuona hapo chini huo ndio mfano wa email ambayo utapokea pale mteja atakapo fanya manunuzi kwenye tovuti yako.

Tengeneza Soko la Mtandaoni Bure Kupitia Blogger (2022)

Kizuri na kwamba zipo huduma nyingi ambazo zinaweza kukusaidia kutuma barua pepe kama SMS, unaweza kupata huduma hizi mtandaoni.

Kama unataka msaada zaidi wa jinsi ya kupata huduma hizo unaweza kuwasiliana nasi tutakusaidia kupata huduma hizo. Pia kama unataka kubadilisha njia za malipo pamoja na sehemu nyingine za muhimu unaweza kuwasiliana nasi kwa msaada zaidi.

Hadi hapo natumaini utakuwa umeweza kutengeneza soko lako la mtandaoni bure kabisa bila kutumia gharama yoyote, Unaweza kununua domain kwa gharama ya TSH 3000 na kuweka kwenye soko lako kwa urahisi.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use