Tumesha zoea kuwa mara nyingi instagram ndio inayochukua baadhi ya sehemu za mtandao wa Snapchat na kuweka kwenye mtandao wake, lakini hivi karibuni Snapchat imeamua kuanza kuchukua sehemu za Instagram kuweka kwenye mtandao wake hasa sehemu ya Stories.
Hivi leo imeripotiwa kuwa, Snapchat inafanyia majaribio ya sehemu mpya ya Mention kwenye sehemu ya Stories kama ilivyo kwenye mtandao wa Instagram. Sehemu hii inafanya kazi sawa na sehemu ya Stories kwenye Instagram. Yaani unaweka alama ya @ na kuweka username ya mtu kwenye picha yako au kwenye sehemu ya maelezo ya picha yako na utakuwa umeweza kumtag mtu kwenye sehemu ya Stories kama ilivyo kwenye instagram.
Utofauti ulipo kwenye sehemu ya mention ya kwenye Snapchat stories ni kuwa, sehemu hii haionyeshi list ya majina pale unapo anza kuandika alama ya “@” kama ilivyo kwenye Instagram, bali itakubidi ukumbuke username kamili ya mtu unaye taka kumtag kwenye sehemu ya Stories kupitia App za Snapchat.
Msemaji wa mtandao wa Snapchat imeambia tovuti ya Tech Crunch kuwa, kwa sasa inafanya majaribio ya sehemu hiyo na bado sehemu hiyo haijaweza kuwezeshwa kwa kila mtumiaji wa mtandao huo. Endelea kutembelea Tanzania Tech kupata Taarifa zaidi kuhusu sehemu hii.