Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Smartphone Aina ya Zuri Zaja Africa Mashariki

Smartphone Aina ya Zuri Zaja Africa Mashariki Smartphone Aina ya Zuri Zaja Africa Mashariki

Kampuni inayotengeneza simu za aina ya ZURI ambayo ina makao makuu yake huko Hong Kong imetangaza kuanza kusambaza bidhaa zake kwa nchi za Afrika Mashariki yani Kenya, Tanzania na Uganda, kampuni hiyo ilitangaza kuungana na kampuni iitwayo Despec ili kufanikisha zoezi hilo la kusambaza simu hizo kwa nchi za afrika mashariki.

Kiongozi wa kampuni hiyo alisema simu ambazo zitakuja kwenye nchi za afrika mashariki ni pamoja na Zuri C41, C46, C52 pamoja na S56. Mwenyekiti huyo Vikash Shah, aliendelea kusema ” nchi za afrika mashariki zinatoa uwezo zaidi wa kukua kwa simu ya ZURI kutoka na kuongezeka kwa mahitaji ya simu za mkononi pia tunaamini kuwa DESPEC ndio mshirika wetu mzuri atakae tusaidia kukua kupitia nchi hizo za afrika mashariki”.

Advertisement

Tukiangalia katika simu hizo za ZURI zinasifa ya kioo cha inch 4.0 kwa simu zake zote ikiwa na RAM ya 512MB mpaka RAM 1GB kwa Zuri C41 hadi S56 pia simu hiyo inauwezo wa Processor ya 1.3 GHz Quad-core hadi processor ya 1.4 GHz Octa-core processo kwa simu zake hizo.

Pia kiongozi wa kampuni ya DESPEC alisema kuwa “tunafurahi kuwa na kampuni ya ZURI kama sehemu ya kampuni yetu, kwani jina la kampuni hii linafanana na ubora wa bidhaa hizo hivyo kampuni hiyo inaonyesha kabisa ya kuwa itapata matokeo mazuri afrika mashariki kutokana na ubora wake” alisema Riyaz Jamal kiongozi wa kampuni hiyo ya DESPEC.

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use