Kama wewe ni mpenzi wa simu za Tecno basi ni matumaini yangu mwaka 2018 umekuwa ni mwaka wa tofauti sana, kwani kampuni hii imebadilika sana hasa kwenye swala zima la muundo wa simu zake. Najua kuwa huwezi kusoma makala zote hapa Tanzania Tech na kuliona hilo leo nitakuleta list ya simu zote mpya za Tecno Zilizotoka mwaka huu 2018.
Simu hizi ni zile tu ambazo zimefika hapa Tanzania au Afrika Mashariki kwa ujumla hivyo usitegemee kuona simu ambazo bado hazijafika hapa Tanzania au Afrika Mashariki kwa ujumla. Kama wewe ni mpenzi wa simu za Tecno ni matumiani yangu kupitia makala hii utaweza kupata simu nzuri ya Tecno ambayo ungependa kuwa nayo kabla ya mwaka 2018 kuisha, basi bila kupoteza muda twende tukangalie list hii.
1. Tecno Camon CM – January 2018
Tecno Camon CM ni moja kati ya simu ya kwanza kwa mwaka huu 2018, Simu hii ilitoka january na ni moja kati ya simu ambayo ukweli inaongoza kwa ubora, Camon CM inakuja na uwezo mzuri sana wa kamera na pia ni simu ngumu sana kati ya simu za Tecno mwaka huu. Camon CM kwa sasa imeshuka bei kidogo lakini bado ni simu nzuri sana kuwa nayo kabla ya mwisho wa mwaka huu 2018. Kwa Sasa unaweza kupata simu hii kwa punguzo hadi Tsh 299,000.
2. Tecno Camon X – April 2018
Baada ya Tecno Kuzindua simu mpya ya Camon CM, miezi mitatu baadae kampuni ya Tecno ilirudi tena na simu mpya ya Camon X pamoja na Camon X Pro. Simu hii ni moja kati ya simu ambayo inapendwa sana na ni moja kati ya simu yenye muonekano mzuri pia simu hii inakuja na sifa ya kuwa simu yenye kamera nzuri hasa ile ya Selfie. Kwa sasa Camon X bado inasimamia kucha na unaweza kuipata kwa punguzo kidogo kuanzia Tsh 400,000.
3. Tecno Pop 1, Tecno F1, Tecno F2 – April 2018
Ukweli ni kuwa soko kubwa la simu linamilikiwa na watumiaji wa kawaida ndio maana kampuni nyingi za simu mwaka huu 2018 zimejikita kuleta simu za bei rahisi ili kukidhi haja za watumiaji hasa wa nchi za Afrika. Kwa sababu hii ndio maana kampuni ya Tecno nayo ilijua na simu za bei rahisi za Tecno Pop 1, Teno F1 pamoja na Tecno F2, Simu hizi ni simu za bei nafuu lakini kwa sasa tayari nazo zinapatikana kwa bei ya punguzo kuanzia Tsh 200,000 kwa Pop 1 na Tsh 170,000 kwa Tecno F1 na Tsh 190,000 kwa Tecno F2.
4. Tecno Spark 2 – June 2018
Mbali ya kutoa simu za bei rahisi bado ilikuwa inaonekana kuwa watu wengi hupendelea simu zenye kufanya kazi kwa haraka ndio maana kampuni ya Tecno ikazindua simu mpya ya Tecno Spark 2 ambayo hii ilikuja na mfumo wa Android GO. Mbali ya kuwa simu hii inakuja na mfumo wenye kufanya kazi kwa haraka pia simu hii ni moja kati ya simu za Tecno za mwaka huu zenye uwezo wa kudumu na chaji kwa muda mrefu. Simu hii ya Spark 2 kwa sasa imeshuka bei kidogo na inakuja kwa punguzo kuanzia Tsh 260,000.
5. Tecno Pouvoir 2 – June 2018
Baada ya kampuni ya Tecno kuzindua simu ya Tecno Spark 2, haikupita siku nyingi kampuni hiyo ilirudi tena kwenye vicha vya habari kwa kuja na simu mpya za Tecno Pouvoir 2 na Tecno Pouvoir 2 Pro. Simu hizi ni maboresho ya simu za Pouvoir 1, Lakini kitu kikubwa kuhusu simu hizi za Pouvoir 2 ni pamoja na uwezo wa simu hii kudumu na chaji kwani simu hizi zinakuja na battery kubwa yenye uwezo wa 5000 mAh ambayo inaweza kudumu siku moja nzima bila wasiwasi, Simu hii kwa sasa bado inasimamia kucha na unaweza kupata kwa punguzo dogo la hadi Tsh 299,000.
6. Tecno Camon 11 – November 2018
Japo kuwa Tecno Camon 11 na Camon 11 Pro ni simu mpya mwezi huu lakini ni wazi kuwa simu hizi ni simu nzuri sana kuwa nazo, simu hizi ni simu za kwanza kabisa kutoka kampuni ya Tecno ambazo zinakuja na ukingo wa juu maarufu kama Notch, pia simu hizi zinafanana sana na muundo wa simu za iPhone X hivyo kama wewe ni mpenzi wa simu hizo basi na uhakika utazipenda simu hizi. Camon 11 Pro inategemewa kuwa bora zaidi kwenye kamera kwani kamera yake inakuja na mfumo wa AI au artificial intelligence.
-
Vipi Kuhusu Phantom ?
Mpaka sasa ni wazi kuwa kampuni ya Tecno bado haijafikiria kutoa simu mpya ya Tecno Phantom, nadhani pengine hii ni katika hali ya kuteka soko kwa kuuza simu za gharama nafuu kwani wote tunajua kuwa simu za Phantom ni simu za bei ghali zaidi kutoka kampuni ya Tecno. Pengine mwakani tegemea kuona simu hii tena ikija na maboresho makubwa sana ikiwa na teknolojia ya AI.
Na hizo ndio Simu za Tecno zilizo toka mpaka sasa mwaka 2018, simu hizi ni ambazo zinatarajiwa kuja au zinakuja kwenye soko hapa Tanzania hivyo pengine inawezekana kuna simu ambayo haipo kwenye list hii pengine hiyo inatokana na simu hiyo kutokwepo kwenye soko la hapa nchini Tanzania au Afrika mashariki kwa ujumla.
Kama kwa namna yoyote unahisi kuna simu ya mwaka huu 2018 ambayo tumesahau kwenye list hii basi unaweza kutukumbusha kupitia kwenye sehemu ya maoni hapo chini.
Umesahau camon 11pro nayo wanazindua siku mbili zijazo
Simu ya mwisho kwenye list