Mamlaka ya mawasiliano tanzania TCRA (Tanzania Communications Regulatory Authority) imetoa tangazo kwa watumiaji wote wa simu za mkononi kwamba, siku ya tarehe 16 ya mwezi juni mwaka huu simu zote za bandia au fake zitafungiwa kutumika tanzania hii ni kwa mujibu wa sheria ya mawasiliano ya kieletroniki na posta kutoka TCRA.
TCRA ilitoa taarifa hizo hivi karibuni, hata hivyo mitandao ya simu kama vile TIGO imesha-anza kutoa huduma hiyo kwa wateja wake ya kuangalia simu za mkononi kama ni bandia. Hii ndio namna ya kuangalia simu yako kama ni badia, huduma hii ilitolewa na mtandao wa TIGO kwenda kwa watumiaji wa simu wa mitandao ya TIGO tu.
- Angalia IMEI kwa kupiga *#06# kisha iandike pembeni.
- Tuma namba hiyo ya IMEI kwenda namba 15090.
- Kisha utapokea taarifa za simu yako kama ni Bandia.
Kumbuka huduma hii inatumia makato ya kawaida ya meseji na pia ni kwa watumiaji wa mtandao wa simu wa TIGO tu. Namna ya kuangalia kama simu yako ni bandia kwa mitandao mingine ya simu tutaendelea kuwafahamisha kadri habari zitakapo tufikia.