Kwa wapenzi wa simu zenye kamera nzuri mwaka huu 2019 ni mwaka wa kukaa kwa kusubiri kwa hamu kwani tegemea kuona au kumiliki simu mpya zenye kamera za Megapixel 64 au Megapixel 100.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka GSMArena, Mkurugenzi mtendaji wa usimamizi wa bidhaa wa kampuni ya Qualcomm, Judd Heape alisema hayo alipokuwa akihojiwa kuhusu processor mpya za Qualcomm snapdragon zinazo tarajiwa kuja hivi karibuni.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa, processor mpya zinazokuja kwa mwaka huu 2019 Snapdragon 865, zinategemewa kuwa na nguvu ya kuweza ku-support kamera za hadi Megapixel 200 huku pia zikisemekana kuwa na uwezo wa teknolojia ya kurekodi video ya HDR10.
Kwa sasa zipo processor za Snapdragon chipsets (660, 670, 675, 710, 845, 855) zinauwezo wa kuwa na kamera hadi Megapixel 192. Baadhi ya simu zenye processor hizi ni pamoja na Xiaomi Mi 9 na Redmi Note 7 Pro ambazo zenyewe zina kamera za hadi Megapixel 48.
Kamera za simu zimezidi kuwa na nguvu kadri siku zinavyo kwenda, hivyo sio kitu cha kushangaza watumiaji wa kamera za kawaida kuamia kwenye kamera za simu kwani ziko simu nyingine ambazo zinakuja na hata kamera za selfie za Megapixel 32 kama ilivyo Huawei Nova 4e iliyozinduliwa hivi karibuni.