Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Hapa Bei za Simu za Tecno Zenye Kamera Nzuri (2019)

Hizi hapa simu za Tecno zenye kamera nzuri hadi sasa
Simu za Tecno zenye kamera nzuri Simu za Tecno zenye kamera nzuri

Ukweli ni kwamba idadi kubwa ya watu hasa hapa Tanzania wanapenda simu mbalimbali kutokana na ubora wake wa kamera. Kwenye upande wa simu za tecno hakuna tofauti sana kwani pia wapenzi wa simu hizi pia wanapendelea ubora wa kamera mbali na sifa nyingine za kawaida.

Kwenye makala hii ya leo tunaenda kuangalia simu za tecno zenye kamera nzuri, pia tunaenda kuangalia bei ya simu hizi vilevile na mahali unapoweza kupata simu hizo. Basi bila kupoteza muda twende tukangalie simu hizo.

Advertisement

10. TECNO Spark 2

Tecno Spark 2 ni simu iliyozinduliwa mwaka huu na ni moja kati ya simu inayokuja na mfumo wa Android GO, mbali na hayo simu hii pia inakuja na kamera nzuri ya Megapixel 8 kwa mbele na Megapixel 13 kwa nyuma. Simu hii inakuja ikiwa inauzwa kwa shilingi za tanzania Tsh 300,000 hadi Tsh 350,000.

Sifa nyingine za Tecno Spark 2

  • Kioo – 6.0-inch IPS Screen display, 720 x 1280 pixels (274 ppi)
  • Processor – 1.3 quad-core with MediaTek MT6580 CPU
  • RAM – GB 2
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.0 yenye HiOS 2.0
  • Ukubwa wa Ndani – GB 16 memory kadi hadi GB 128
  • Kamera ya Mbele – Megapixel 8
  • Kamera ya Nyuma – Megapixel 13
  • Uwezo wa Mtandao – 4G LTE (up to 150Mbps)
  • Ulinzi – Fingerprint Sensor (Kwa nyuma)
  • Uwezo wa Battery – 3500 mAh Battery yenye Fast Charging

9. TECNO Camon CX Air

Tecno Camon CX Air sio simu ya muda sana kutoka kampuni ya Tecno, simu hii imezinduliwa mwaka jana na ni moja kati ya simu za Tecno inayokuja na kamera nzuri sana. Simu hii inakuja na kamera ya mbele ya Megapixel 13 vilevile na nyuma pia inakuja na kamera yenye uwezo huohupo wa Megapixel 13. Simu hii inapatikana kwa bei ya Tsh 290,000 hadi Tsh 350,000.

Sifa za nyingine Tecno Camon CX Air

  • Kioo – 5.5-inch IPS Screen display, 720 x 1280 pixels (267 ppi)
  • Processor – 1.25GHz quad-core with MediaTek MT6737 CPU
  • RAM – GB 2
  • Mfumo wa Unendeshaji – Android 7.0 yenye HiOS 2.0
  • Ukubwa wa Ndani – GB 16 memory kadi hadi GB 128
  • Kamera ya Mbele – Megapixel 13
  • Kamera ya Nyuma – Megapixel 13
  • Uwezo wa Mtandao – 4G LTE (up to 150Mbps)
  • Ulinzi – Fingerprint Sensor (Kwa nyuma)
  • Uwezo wa Battery – 3200 mAh Battery yenye Fast Charging

8. TECNO Camon CM

Moja kati ya simu ya mwaka huu inayofanya vizuri sana ni simu hii ya Tecno Camon CM, simu hii inakuja na muundo mzuri lakini pia inakuja na kamera nzuri sana. Camon Cm inakuja ikiwa na kamera ya Megapixel 13 kwa mbele na nyuma. Simu hii inakuja kwa bei ya kuanzia Tsh 300,000 hadi Tsh 400,000.

Sifa Nyingine za Tecno Camon CM

  • Kioo – 5.65-inch IPS Screen display, 720 x 1280 pixels (267 ppi)
  • Processor – 1.3GHz quad-core with MediaTek MT6737H CPU
  • RAM – GB 2
  • Mfumo wa Unendeshaji – Android 7.0 yenye HiOS 2.0
  • Ukubwa wa Ndani – GB 16 memory kadi hadi GB 128
  • Kamera ya Mbele – Megapixel 13
  • Kamera ya Nyuma – Megapixel 13
  • Uwezo wa Mtandao – 4G LTE (up to 150Mbps)
  • Ulinzi – Fingerprint Sensor (Kwa nyuma)
  • Uwezo wa Battery – 3050 mAh Battery

7. TECNO Camon CX Manchester Edition

Simu hii ni toleo maalum ambalo kampuni ya Tecno iliungana na klabu ya mpira ya Manchester United na muungano huo ulizalisha toleo la simu hii ambayo nayo inakuja na uwezo mzuri sana wa kamera. Kama wewe ni mpenzi wa simu nzuri za tecno zenye kamera nzuri basi pia simu hii ni bora sana kuwa nayo. Tecno Camon CX Manchester Edition inakuja na Kamera ya mbele ya Megapixel 16 na kamera ya nyuma nayo pia inakuja na Megapixel 16. Simu hii inauzwa kwa kati ya Tsh 300,000 hadi Tsh 450,000.

Sifa nyingine za Tecno Camon CX Manchester Edition

  • Kioo – 5.5-inch IPS Screen display, 1920 X 1080 pixels
  • Processor – Octa-Core Cortex A53,1.5GHz,  MediaTek MT6750T CPU
  • RAM – GB 4
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 yenye HiOS 2.0
  • Ukubwa wa Ndani – GB 64 memory kadi hadi GB 128
  • Kamera ya Mbele – Megapixel 16
  • Kamera ya Nyuma – Megapixel 16
  • Uwezo wa Mtandao – 4G LTE (up to 150Mbps)
  • Ulinzi – Fingerprint Sensor (Kwa nyuma)
  • Uwezo wa Battery – 3200 mAh Battery yenye Fast Charging

6. TECNO Camon CX

Kama ilivyo simu ya Tecno Camon CX Manchester Edition, simu hii ya Camon CX nayo pia inakuja na kamera nzuri sana ya mbele pamoja na nyuma. Simu hii inakuja na kamera zote za mbele na nyuma zenye uwezo wa Megapixel 16. Simu hii inakuja kwa bei ya Tsh 300,000 hadi 400,000.

Sifa nyingine za Tecno Camon CX

  • Kioo – 5.5-inch IPS Screen display, 1080 x 1920 ・pixels (400 ppi)
  • Processor – 1.5GHz octa-core, Mediatek MT6750T CPU
  • RAM – GB 2
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 yenye HiOS 2.0
  • Ukubwa wa Ndani – GB 16 memory kadi hadi GB 128
  • Kamera ya Mbele – Megapixel 16
  • Kamera ya Nyuma – Megapixel 16
  • Uwezo wa Mtandao – 4G LTE (up to 300Mbps)
  • Ulinzi – Fingerprint Sensor (Kwa nyuma)
  • Uwezo wa Battery – 3200 mAh Battery yenye Fast Charging

5. TECNO Camon X

Tecno Camon X ni simu nyingine nzuri sana kwa upande wa kamera, simu hii imezinduliwa hivi karibuni na ni moja kati ya simu za mwaka huu kutoka kampuni ya Tecno yenye ubora wa kamera hasa kwenye kamera ya mbele. Simu hii inakuja na kamera ya mbele ya Megapixel 20 na kamera ya nyuma inakuja na Megapixel 13, simu hii inakuja ikiwa na bei ya Tsh 300,000 hadi Tsh 450,000.

Sifa nyingine za Tecno Camon X

  • Kioo – 6.0-inch IPS Screen display, 1080 x 2160 ・pixels (269 ppi)
  • Processor – 2.0GHz octa-core, Mediatek Hello P23 CPU
  • RAM – GB 3
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 yenye HiOS 2.0
  • Ukubwa wa Ndani – GB 16 memory kadi hadi GB 128
  • Kamera ya Mbele – Megapixel 20
  • Kamera ya Nyuma – Megapixel 13
  • Uwezo wa Mtandao – 4G LTE (up to 300Mbps)
  • Ulinzi – Fingerprint Sensor (Kwa nyuma)
  • Uwezo wa Battery – 3750 mAh Battery

4. TECNO Camon X Pro

Kama ilivyo simu ya Tecno Camon X simu hii pia inakuja na sifa sawa na Tecno Camon X, lakini kwa upande wa kamera simu hii inakuja ikiwa na kamera nzuri zenye uwezo wa Megapixel 24 kwa mbele na kamera ya Megapixel 13 kwa kamera ya nyuma. Simu hii inakuja ikiwa inauzwa kati ya Tsh 350,000 hadi Tsh 600,000.

Sifa nyingine za Tecno Camon X Pro

  • Kioo – 6.0-inch IPS Screen display, 1080 x 2160 ・pixels (269 ppi)
  • Processor – 2.0GHz octa-core, Mediatek Hello P23 CPU
  • RAM – GB 4
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 yenye HiOS 2.0
  • Ukubwa wa Ndani – GB 16 memory kadi hadi GB 128
  • Kamera ya Mbele – Megapixel 24
  • Kamera ya Nyuma – Megapixel 13
  • Uwezo wa Mtandao – 4G LTE (up to 300Mbps)
  • Ulinzi – Fingerprint Sensor (Kwa nyuma)
  • Uwezo wa Battery – 3750 mAh Battery

3. Tecno Camon 11 Pro

Kizuri kuhusu Tecno Camon 11 na Camon 11 pro

Mwishoni mwa Mwaka 2018 kampuni ya Tecno imezindua simu mbili mpya za Tecno Camon 11 na Camon 11 Pro, simu hizi ni moja ya simu ambazo kwa kweli zinajitahidi sana kwa upigaji picha wake kwani simu hizi ni simu za kwanza kabisa kutoka kampuni ya Tecno kuja na teknolojia ya AI kwenye kamera zake. Hivyo basi kama unapenda kamera basi simu hizi ni bora sana kwa mwaka huu.

Sifa nyingine za Tecno Camon 11 Pro

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.2 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1500 pixels, na uwiano wa 19:9 ratio (~269 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo) na HiOS 4.1
  • Uwezo wa Processor – Octa-Core 2.0GHz.
  • Aina ya Processor (Chipset) – MediaTek Helio P22 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Mali-G71 MP2.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 128.
  • Ukubwa wa RAM – GB 6.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 24 yenye teknolojia ya AI pamoja na LED Flash

2. TECNO Phantom 8

Moja kati ya simu ya bora kutoka kampuni ya Tecno ni Tecno Phantom 8, simu hii inakuja na muonekano mzuri sana na mbali na hayo simu hii inapiga picha vizuri pengine kuliko simu nyingine kutoka Tecno kwa sasa. Simu hii inakuja na kamera ya mbele ya Megapixel 20 na kwa nyuma inakuja na kamera mbili zenye Megapixel 12 na Megapixel 13. Simu hii inakuja na bei kati ya Tsh 600,000 hadi Tsh 900,000.

Sifa nyingine za Tecno Phantom 8

  • Kioo – 5.7-inch IPS Screen display, 3840 x 2160 pixels
  • Processor – 2.6GHz octa-core,MediaTek MT6557CDCPU
  • RAM – GB 6
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 yenye HiOS 3.0
  • Ukubwa wa Ndani – GB 64 memory kadi hadi GB 500
  • Kamera ya Mbele – Megapixel 20
  • Kamera ya Nyuma – Megapixel 13 na Megapixel 12
  • Uwezo wa Mtandao – 4G LTE (up to 400Mbps)
  • Ulinzi – Fingerprint Sensor (Kwa nyuma)
  • Uwezo wa Battery – 3500 mAh Battery

1. TECNO Phantom 8 Plus

Kwa upande wa toleo la Phantom 8 Plus, simu hii inafanana sana kamera na simu ya Phantom 8, lakini kwa upande wa sifa nyingine simu hii inakuja na uwezo mkubwa zaidi. Kuhusu bei simu hii pia inakuja kwa bei ghali zaidi na inaweza kukadiriwa kuanzia Tsh 600,000 na Tsh Tsh 100,000,000.

Sifa nyingine za Tecno Phantom 8 Plus

  • Kioo – 5.7-inch IPS Screen display, 3840 x 2160 pixels
  • Processor – 2.6GHz octa-core,MediaTek MT6557CDCPU
  • RAM – GB 6
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 yenye HiOS 3.0
  • Ukubwa wa Ndani – GB 128 memory kadi hadi GB 500
  • Kamera ya Mbele – Megapixel 20
  • Kamera ya Nyuma – Megapixel 13 na Megapixel 12
  • Uwezo wa Mtandao – 4G LTE (up to 400Mbps)
  • Ulinzi – Fingerprint Sensor (Kwa nyuma)
  • Uwezo wa Battery – 4000 mAh Battery

Na hizo ndio simu za Tecno ambazo zinakuja na kamera nzuri hadi sasa. Kama unafahamu simu nyingine ya Tecno ambayo tumeisahau kwenye list hii unaweza kutuandikia kwenye maoni hapo chini nasi tutaiongeza simu hiyo kwenye list hii. Kama unatafuta simu nyingine bora za Tecno unaweza kusoma hapa.

2 comments
  1. Nakubali sana sm ya tecno but sm yangu sahv hii nayotumia inaresponding nifanyeje jina lake tecno spark k7 naomba msaada

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use