Simu za Tecno ni moja kati ya simu zinazotumiwa na watu wengi sana hapa Tanzania na Afrika kwa ujumla, Simu hizi zimekuwa zikitumiwa na watu wengi kwa sababu ya unafuu wake wa bei na hivyo kurahisisha mawasiliano miongoni mwa watumiaji wengi wa simu hizi.
Kuliona hili leo Tanzania Tech tunakuletea list ya simu za Tecno za bei rahisi, ikiwa pamoja na sifa za simu hizo pamoja na sehemu unazoweza kununua simu hizo kwenye maduka mbalimbali au kupitia mitandao mbalimbali. Vilevile kwenye list hii tutaenda kuangalia simu za tecno za bei rahisi ambazo ni kati ya shilingi za kitanzania Tsh 250,000 hadi Tsh 300,000. Basi bila kupoteza muda twende tukaangalie list hii ya simu hizi za bei nafuu.
1. TECNO L8 Lite
Simu ya Tecno L8 Lite ni moja kati ya simu za tecno za bei rahisi, simu hii inakuja na sifa za kawaida huku ikiwa na uwezo wa kudumu na chaji kwa muda mrefu kutokana na ukubwa wa battery yake yenye uwezo wa 4,000mAh, sifa nyingine za simu hii ni kama zifuatazo.
TABLE OF CONTENTS
Sifa za Tecno L8 Lite
- Ukubwa wa Kioo – Inch 5.0 chenye teknolojia ya IPS Capacitive Touchscreen
- Ukubwa wa Ndani – GB 16
- Ukubwa wa RAM – GB 1
- Kamera ya Mbele – Megapixel 2
- Kamera ya Nyuma – Megapixel 8
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 6.0 Marshmallow
- Uwezo wa Battery – 4000mAh Li-Ion
- BEI – 200,000 – 250,000
2. TECNO F2
Tecno F2 ni moja kati ya simu ambazo pia ni simu za bei nafuu kutoka kampuni ya Tecno, simu hii imezinduliwa hivi karibuni na inakuja na mfumo wa Android Nougat pamoja na sifa nyingine kama zifuatazo.
Sifa za Tecno F2
- Ukubwa wa Kioo – Inch 5.0 chenye teknolojia ya IPS Capacitive Touchscreen
- Ukubwa wa Ndani – GB 8
- Ukubwa wa RAM – GB 1
- Kamera ya Mbele – Megapixel 2
- Kamera ya Nyuma – Megapixel 8
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 Nougat
- Uwezo wa Battery – 2000mAh Li-Ion
- BEI – 150,000 – 250,000
3. TECNO Pop 1
Tecno Pop 1 ni simu ya bei nafuu ya tecno ambayo nayo pia ilizinduliwa sambamba na simu ya Tecno F2, Simu hii inakuja na kioo kikubwa na ni moja kati ya simu nzuri na za bei nafuu kutoka kampuni ya Tecno.
Sifa za Tecno Pop 1
- Ukubwa wa Kioo – Inch 5.5 chenye teknolojia ya qHD IPS Capacitive Touchscreen
- Ukubwa wa Ndani – GB 8
- Ukubwa wa RAM – GB 1
- Kamera ya Mbele – Megapixel 2
- Kamera ya Nyuma – Megapixel 8
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 Nougat
- Uwezo wa Battery – 2500mAh Li-Ion
- BEI – 190,000 – 250,000
4. TECNO Spark K7
Simu nyingine ya Bei nafuu kutoka Tecno ni simu ya Tecno Spark K7, simu hii ni nzuri sana kwa umbo lake na pia ni moja kati ya simu zenye kamera nzuri kutoka na yenye uwezo wa kudumu na chaji. Sifa nyingine za Tecno Spark K7 ni kama zifuatazo.
Sifa za Tecno Spark K7
- Ukubwa wa Kioo – Inch 5.5 chenye teknolojia ya qHD IPS Capacitive Touchscreen
- Ukubwa wa Ndani – GB 8
- Ukubwa wa RAM – GB 1
- Kamera ya Mbele – Megapixel 5
- Kamera ya Nyuma – Megapixel 13
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 Nougat
- Uwezo wa Battery – 3000mAh Li-Ion
- BEI – 200,000 – 300,000
5. TECNO WX4
Simu nyingine ya bei rahisi ni Tecno WX4, simu hii ya tecno inakuja na kioo kikubwa cha inch 5.0 pamoja na uwezo mzuri wa battery. Sifa nyingine za Tecno WX4 ni kama zifuatazo.
Sifa za Tecno WX4
- Ukubwa wa Kioo – Inch 5.0 chenye teknolojia ya HD IPS Capacitive Touchscreen
- Ukubwa wa Ndani – GB 16
- Ukubwa wa RAM – GB 1
- Kamera ya Mbele – Megapixel 8
- Kamera ya Nyuma – Megapixel 8
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 Nougat
- Uwezo wa Battery – 2800mAh Li-Ion
- BEI – 290,000 – 300,000
6. TECNO WX3
Tecno wx3 pia ni simu nyingine ya bei nafuu kutoka kampuni ya Tecno. Simu hii inakuja na uwezo wa kawaida na ni simu nzuri sana kwa wale wanaotaka kwenda na bajeti. Sifa za Tecno Wx3 ni kama zifuatazo.
Sifa za Tecno WX3
- Ukubwa wa Kioo – Inch 5.0 chenye teknolojia ya IPS Capacitive Touchscreen
- Ukubwa wa Ndani – GB 8
- Ukubwa wa RAM – GB 1
- Kamera ya Mbele – Megapixel 5
- Kamera ya Nyuma – Megapixel 5
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 Nougat
- Uwezo wa Battery – 2300mAh Li-Ion
- BEI – 250,000 – 300,000
7. TECNO R6
Simu ya Tecno R6 ni moja kati ya simu zinazojulikana sana hapa Tanzania, mbali na kujulikana simu hii pia ni ya bei nafuu sana na inakuja na sifa zifuatazo.
Sifa za Tecno R6
- Ukubwa wa Kioo – Inch 5.0 chenye teknolojia ya IPS Capacitive Touchscreen
- Ukubwa wa Ndani – GB 8
- Ukubwa wa RAM – GB 1
- Kamera ya Mbele – Megapixel 2
- Kamera ya Nyuma – Megapixel 5
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 6.0 Mashmalow
- Uwezo wa Battery – 2300mAh Li-Ion
- BEI – 150,000 – 300,000
8. TECNO Spark 2
Simu nyingine ya tecno ya bei rahisi ni Tecno spark 2, simu hii imezinduliwa hivi karibuni na inakuja na uwezo mzuri wa kamera pamoja na kioo kikubwa bila kusahau mfumo wa Android Go. Sifa nyingine za Tecno spark 2 ni kama zifuatazo.
Sifa za Tecno Spark 2
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.0 chenye teknolojia ya IPS Capacitive Touchscreen
- Ukubwa wa Ndani – GB 16
- Ukubwa wa RAM – GB 1
- Kamera ya Mbele – Megapixel 8
- Kamera ya Nyuma – Megapixel 13
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 Oreo GO Edition
- Uwezo wa Battery – 3500mAh Li-Ion
- BEI – 250,000 – 300,000
9. TECNO Spark K8
Tecno spark k8 ni simu ya bei nafuu sana kutoka kampuni ya Tecno, simu hii inakuja na muundo muzri lakini mbali na hayo simu hii inakuja na uwezo wa mtandao wa 4G pamoja na kamera nzuri na battery inayodumu na chaji zaidi. Sifa nyingine za Tecno Spark K8 ni kama zifuatazo.
Sifa za Tecno Spark K8
- Ukubwa wa Kioo – Inch 5.5 chenye teknolojia ya IPS Capacitive Touchscreen
- Ukubwa wa Ndani – GB 16
- Ukubwa wa RAM – GB 1
- Kamera ya Mbele – Megapixel 5
- Kamera ya Nyuma – Megapixel 13
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 Nougat
- Uwezo wa Battery – 3000mAh Li-Ion
- BEI – 290,000 – 300,000
10. TECNO Spark 3 (3G)
Tecno spark 3 ni simu nzuri na ya bei nafuu kutoka kampuni ya Tecno, simu hii imezinduliwa hivi karibuni na inakuja na sifa bora na nzuri sana. Mbali na hayo simu hii imeboreshwa sana upande wa kamera kwani inakuja na kamera zenye mfumo wa AI pamoja na uwezo mkubwa wa kupiga picha hasa wakati wa usiku, sifa za tecno spark 3 ni kama zifuatazo.
Sifa za Tecno Spark 3
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.4 chenye teknolojia ya IPS LCD Capacitive Touchscreen
- Ukubwa wa Ndani – GB 16
- Ukubwa wa RAM – GB 2
- Kamera ya Mbele – Megapixel 8
- Kamera ya Nyuma – Megapixel 13 na Megapixel 2
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 Pie
- Uwezo wa Battery – 3500mAh Li-po
- BEI – 290,000 – 300,000
Na hizo ndio simu za tecno za bei rahisi kwa sasa, unaweza kupata simu hizi kupitia maduka mbalimbali ya Tecno hapa Tanzania. Pia unaweza kupata simu nyingine za nzuri za tecno zenye kamera nzuri kwa kusoma makala hii hapa. Kama unahisi kuna simu yoyote ya tecno ya bei rahisi tuliyo isahau kwenye list hii unaweza kutuandikia kwenye sehemu ya maoni hapo chini.
Tecno K 9 bei gani
Simu za batani je
naomba taarifa ya tecno mpya zilizotoka 2018
Erekebishen kwenye inside memory na kwenye ram sim ina uzwa laki 3 kisha ram 1GB MEMORY 8BG LAKI 3 SIO NDOGO ATIRIST IWE NA RAM 3GB MEMORY 16GB
Hakika Simu ni zuri na bei yake ipo vizuri tu tatizo linakuja unapo kwenda dukani kununua unakuta bei tofauti na hii iliyoandikwa mtandaoni inakuwaje? Pili mbona Simu hizi za Tecno zinastak Mara kwa Mara nini tatizo ?
Napongeza sana jinsi mnavyotujuzaa ningependa kushauli muwe na matawi ya hizi Bidhaa mikoani being Ni nzur na itasaidiaa sana mkoani Leo Niko Chunya wilayani kesho naenda MBEYA mjini nitazipata WAP?
Habari za saizi Mimi nasikitika sana kuwa campuni za kutengeneza simu hapa Zanzibar hamjaweka matawi kama Tanzania bara