Tumeshaongelea sana simu bora za TECNO, lakini ukweli ni kwamba japo kuwa TECNO inatoa simu mpya kiribia kila mwezi lakini bado simu hizi nyingi hazina sifa na ubora kama baadhi ya simu ambazo kampuni ya tecno ilishawahi kuzindua.
Leo nimekuletea list hii fupi ya simu za zamani za tecno ambazo zinaubora mpaka sasa, simu nilizo kuwekea kwenye list hii zinaubora sana japokuwa zimezinduliwa ndani ya miaka miwili au mitatu iliyopita. Kwa wengine najua mtasema simu za sasa ni bora lakini mwishoni kabisa nitaweza kukwambia kwanini mimi binafsi naona simu hizo za zamani ni bora kuliko za sasa, basi bila kupoteza muda let’s get to it.
TABLE OF CONTENTS
TECNO Phantom 8
TECNO Phantom 8 sio simu ya siku nyingi sana lakini ni muhimu kuitaja kwenye list hii kwani simu hii ina umri zaidi ya mwaka mmoja sasa. Phantom 8 ni simu ambayo ilitengenezwa kwa muundo mzuri sana na ni moja kati ya simu za awali kutoka kampuni ya TECNO kuja na kamera mbili kwa nyuma. Mbali ya hayo simu hii inakuja na kamera nzuri sana yenye uwezo mzuri sana pamoja na uwezo wa kuchukua video za hadi 2160p@30fps. Simu hii pia ni moja kati ya simu za kwanza kutoka tecno zilizokuwa na RAM ya hadi GB 6, yaani inaweza kushindana na simu mpya ya TECNO Camon 11 na Camon 11 Pro za mwaka (2018).
Sifa za TECNO Phantom 8
- Kioo – inch 5.7 inches chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen
- Kamera – Mbili kwa nyuma zenye Megapixel 13 na Megapixel 12
- Processor – Octa-core 2.0 GHz Cortex-A53 yenye chip ya Mediatek MT6757T Helio P25 (16 nm)
- RAM – GB 6
- Ukubwa wa ROM – GB 64.
Kwa sasa TECNO Phantom 8 inapatikana kwenye maduka mbalimbali ya TECNO na inapatikana kwa bei kati ya Tsh 600,000 hadi Tsh 800,000.
TECNO Phantom 6 Plus
TECNO Phantom 6 ni simu nyingine ambayo ni bora sana hadi sasa, Simu hii inakuja kioo bora ambacho pia kina ulinzi wa Corning Gorilla Glass 3. Mbali ya kuwa na kioo bora simu hii pia inakuja na uwezo mkubwa sana kwenye kamera huku ikiwa na uwezo wa kuchukua video hadi za 2160p@30fps. Mbali ya yote uzuri wa simu hii haupo kwenye vitu hivyo pekee, simu hii ni moja kati ya simu pekee za TECNO yenye processor kubwa za Deca Core. Processor hii ina nguvu na hadi sasa inatumika kwenye simu chache sana.
Sifa za TECNO Phantom 6 Plus
- Kioo – inch 6.0 inches chenye teknolojia ya LTPS IPS LCD capacitive touchscreen
- Kamera – Moja kwa nyuma yenye Megapixel 21
- Processor – Deca-core 2.0 GHz yenye chip ya Mediatek MT6797 Helio X20 (20 nm)
- RAM – GB 4
- Ukubwa wa ROM – GB 64.
Kwa sasa TECNO Phantom 6 Plus nayo imetoweka lakini kama ukipata simu hii ikiwa mpya unaweza kuipata kwa Tsh 600,000 hadi Tsh 750,000.
TECNO Phantom 6
Japokuwa TECNO phantom 6 imetoka miaka kadhaa iliyopita lakini kwangu mimi itabaki kuwa simu bora kutoka kampuni ya TECNO. Ubora wa simu hii kwa upande wangu ni kioo, simu hii ni moja kati ya simu chache sana na TECNO ambazo zimewahi kuwa na kioo kikubwa cha namna hii chenye ulinzi wa Corning Gorilla Glass 3.
Kifupi ni kuwa katika swala la kioo bora Phantom 6 ni moja kati ya simu iliyokuwa na kioo bora sana chenye teknolojia ya kisasa. Kwa upande wa sifa Phantom 6 ni kama simu nyingine za TECNO ambazo zimezinduliwa hivi karibuni.
Sifa za TECNO Phantom 6
- Kioo – inch 5.5 inches chenye teknolojia ya AMOLED capacitive touchscreen
- Kamera – Mbili kwa nyuma zenye Megapixel 13 na Megapixel 5
- Processor – Octa-core 2.0 GHz Cortex-A53 yenye chip ya Mediatek MT6755 (28 nm)
- RAM – GB 3
- Ukubwa wa ROM – GB 32.
Kwa sasa TECNO Phantom 6 haipatikani sana, ila unaweza kuipata kwa bei ya kuanzia Tsh 500,000 hadi 600,000.
TECNO Camon CX Manchester City Limited Edition
TECNO Camon CX Manchester Edition ni moja kati ya simu nzuri sana hadi sasa, mbali ya kuwa limited edition simu hii pia inakuja na RAM zaidi na ukubwa wa ROM zaidi kuliko toleo la kawaida la TECNO camon CX. Mbali ya yote TECNO Camon CX Manchester Edition ni moja kati ya simu yenye uwezo mkubwa sana wa batter pamoja na teknolojia ya Fast Charging.
Sifa za TECNO Camon CX Manchester Edition
- Kioo – inch 5.5 inches chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen
- Kamera – Moja kwa nyuma yenye Megapixel 13
- Kamera ya Mbel – Mgeapixel 13
- Processor – Octa-Core Cortex A53 1.5GHz yenye chip ya MediaTek MT6750T
- RAM – GB 4
- Ukubwa wa ROM – GB 64.
TECNO Camon CX Manchester City Limited Edition kwa sasa unaweza kuipata kwenye maduka mbalimbali ya TECNO kwa shilingi za kitanzania Tsh 350,000 hadi 400,000
TECNO L9 plus
TECNO L9 Plus ni moja kati ya simu nzuri sana kutoka TECNO, simu hii mbali ya uzuri wake pamoja na sifa, simu hii inaweza ikawa moja kati ya simu ya tecno yenye kudumu na chaji kwa muda mrefu sana. Simu hii inakuja na battery kubwa ya 5000 mAh ambayo inaweza kukupa zaidi ya siku moja nzima kwa matumizi ya kawaida ya simu yako.
Sifa za TECNO L9 Plus
- Kioo – inch 5.6 inches chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen
- Kamera – Moja kwa nyuma yenye Megapixel 13
- Kamera ya Mbel – Mgeapixel 5
- Processor – Quad-core 1.3GHz yenye chip ya MediaTek
- RAM – GB 3
- Ukubwa wa ROM – GB 16.
Kwa sasa simu hii imepotea kidogo lakini ukipata simu hii unaweza kuuziwa kwa kati ya Tsh 250,000 hadi Tsh 350,000.
Na hizo ndio simu ambazo binafsi naona ni za zamani lakini zinaweza kushindana na baadhi ya simu ambazo ziko sokoni kwa sasa. Nikirejea kwenye sababu kwanini simu hizi zina ubora ni kuwa, kampuni ya TECNO kwa mwaka 2018 imeonekana kuzingatia zaidi kamera kuliko sifa za simu, lakini ukiangalia simu hizi kwenye list hii sio ubora pekee wa kamera bali pia simu hizi pia zinakuja na sifa nzuri sana ukitofautisha na simu nyingi mpya za Tecno za mwaka 2018.
Kifupi haya ni maoni yangu binafsi, je wewe unaonaje kwenye list hii..? kuna simu ambayo unahisi inastahili kuwepo hapa na nimeisahau..? tuambie kwenye sehemu ya moani hapo chini.
vipi kuhusu Tecno c8 mbona nayo ilikuwa ya ukweli
Nina tecno povour lakin imeharibika kioo kwenye maduka yenu naweza kupata kioo na kwa bei gan??