Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Hapa Simu za Infinix za Bei Rahisi kwa Mwaka (2020)

Kama unatafuta simu za infinix za bei nafuu basi hii hapa list ya simu hizo
Hizi Hapa Simu za Infinix za Bei Rahisi kwa Mwaka (2020) Hizi Hapa Simu za Infinix za Bei Rahisi kwa Mwaka (2020)

Infinix ni moja kati ya simu ambazo zinatumiwa na watu wengi sana, siku za karibuni kampuni hiyo imekuwa ikizindua simu bora za bei nafuu ambazo pia zinakuja na sifa bora sana. Kuliona hili leo nimekuletea list ya simu za bei rahisi kutoka kampuni ya Infinix, natumaini list hii itakusaidia kupata simu bora kwa bei nafuu.

Kumbuka bei za simu hizi zinaweza kuwa tofauti kulingana na eneo ambalo unapatikana, pia kama unataka kujua sifa za simu hizi unaweza kubofya link chini ya simu husika. Basi bila kuendelea kupoteza muda twende moja kwa moja kwenye list hii.

Advertisement

Infinix Hot 8 – TZS 280,000

Hizi Hapa Simu za Infinix za Bei Rahisi kwa Mwaka (2020)

Infinix Hot 8 ni moja kati ya simu bora na simu ya bei rahisi hasa kama wewe ni mmoja wa watu wanaopenda simu zinazo dumu na chaji, simu hii ni bora sio kwa upande wa chaji tu bali pia simu hii inakuja na muonekano mzuri na pia simu hii inakuja na mfumo mpya wa Android 9.0 (Pie) pamoja na mfumo wa infinix wa XOS 5.5.

  • CPU: Octa-core 2.0 GHz
  • RAM: 4 GB
  • Storage: 64 GB
  • Display: IPS LCD 6.5 Inch
  • Camera: Triple 13 MP, 2 MP, 2MP
  • OS: Android 9.0 (Pie)

Infinix Hot 8 Lite – TZS 260,000

Hizi Hapa Simu za Infinix za Bei Rahisi kwa Mwaka (2020)

Tofauti kidogo na Infinix Hot 8, infinix Hot 8 Lite nayo ni simu nzuri sana ambayo inapatikana kwa bei nafuu chini ya TZS 300,000. Simu hii ni bora sana kwa wale ambao wanataka simu nzuri ya kisasa yenye uwezo wa kawaida. Simu hii inakuja na mfumo wa Android Go, mfumo ambao ni maalum kwa simu zenye uwezo wa RAM chini ya GB 1.

  • CPU: Quad-core 1.3 GHz
  • RAM: 1 GB
  • Storage: 32 GB
  • Display: IPS LCD 6.6 Inch
  • Camera: Dual 8 MP, QVGA
  • OS: Android 8.1 Oreo (Go edition)

Infinix Smart 3 Plus – TZS 280,000

Hizi Hapa Simu za Infinix za Bei Rahisi kwa Mwaka (2020)

Kama wewe ni mpenzi wa simu ya infinix yenye muonekano bora na sifa za nzuri simu hii ya infinix smart 3 Plus ni simu bora sana kwako. Simu hii kama simu zilizopita kwenye list hii ni simu bora sana ambayo unaweza kupata kwa bei nafuu chini ya Shilingi za kitanzania TZS 300,000.

  • CPU: Quad-core 2.0 GHz Cortex-A53
  • RAM: 2/3 GB
  • Storage: 16/32 GB
  • Display: IPS LCD, 6.2 inches
  • Camera: Triple 13MP, 2MP, QVGA
  • OS: Android 9.0 (Pie)

Infinix Smart 3 – TZS 260,000

Hizi Hapa Simu za Infinix za Bei Rahisi kwa Mwaka (2020)

Kama ilivyo infinix hot 8 lite, infinix smart 3 ni toleo la bei rahisi zaidi kwenye simu hizi za Smart 3, simu hii pia ni simu ambayo unaweza kupata kwa bei rahisi na ni moja kati ya simu ambazo zina muonekano mzuri pamoja na sifa nzuri pia. Simu hii pia inakuja na mfumo wa Android 9.0 (Pie) Go mfumo ambao ni maalum kwa simu zenye RAM chini ya GB 1.

  • CPU: Quad-core 2.0 GHz Cortex-A53
  • RAM: 2 GB
  • Storage: 16 GB
  • Display: IPS LCD, 5.5 inches
  • Camera: Dual 13MP, 2MP
  • OS: Android 9.0 (Pie) Go Edition

Infinix S5 Lite – TZS 270,000

Hizi Hapa Simu za Infinix za Bei Rahisi kwa Mwaka (2020)

Infinix S5 Lite ni toleo jipya la simu mpya za Infinix S5, simu hii inakuja na muonekano mzuri na ni moja kati ya simu za bei rahisi kutoka kampuni ya Infinix. Simu hii inakuja na uwezo mzuri wa RAM pamoja na kamera tatu kwa nyuma ambazo zinaweza kuchukua picha vizuri sana kwa kusaidiwa na teknolojia ya AI.

  • CPU: Octa-core CPU (4×2.0 GHz Cortex-A53 and 4×1.5 GHz Cortex-A53)
  • RAM: 6/4 GB
  • Storage: 32/64 GB
  • Display: IPS LCD, 6.6 inches
  • Camera: Triple 16 MP, 2 MP, QVGA
  • OS: Android 9.0 (Pie)

Infinix Note 7 Lite – TZS 300,000

Hizi Hapa Simu za Infinix za Bei Rahisi kwa Mwaka (2020)

Infinix Note 7 Lite ni simu mpya kabisa kutoka kampuni ya Infinix, mbali ya kuwa simu hii inakuja na muonekano mpya na wa kisasa lakini pia simu hii inakuja na sifa nzuri sana tofauti na simu nyingi kwenye list hii. Simu hii inakuja na RAM ya GB 4 pamoja na kamera nne kwa nyuma. Kama wewe ni mmoja wa watu wanao tafuta simu bora yenye sifa nzuri kwa bei rahisi basi Note 7 lite ni simu.

  • CPU: Octa-core (2×2.0 GHz Cortex-A75 & 6×1.7 GHz Cortex-A55)
  • RAM: 4 GB
  • Storage: 64/128 GB
  • Display: IPS LCD, 6.6 inches
  • Camera: Quad 48 MP, 8 MP, 2 MP, QVGA
  • OS: Android 10.0

List inaendelea…

Kwa sasa hizo ndio simu za bei rahisi kutoka kampuni ya Infinix, kama unataka kujua simu zaidi za infinix za bei rahisi unaweza kuendelea kutembelea makala hii kwani tutakuwa tukiongeza simu mpya kadri zinavyo endelea kutoka kila siku.

Kama unataka kujua sifa na bei ya simu zote mpya zitakazo toka kwa hapa Tanzania, unaweza kusoma kipengele cha simu mpya na utapata taarifa pindi tu simu mpya zitakapo zinduliwa.

1 comments
  1. Naomba kujua Infinx note 7 inapatikana wapi hapa Dar es salaam ,kwa bei iyo ? Nina shida nayo. Sana

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use