Heri ya Mwaka Mpya 2022, Lakini kwa watumiaji wa simu za zamani za Blackberry pengine inaweza kuwa kama mwaka umeanza vibaya.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kampuni ya Blackberry, simu za zamani za blackberry ambazo zinatumia mfumo wa zamani wa BlackBerry 10 au BlackBerry 7.1 na kuendelea hazitoweza kutumika tena kuanzia January 4.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Kuanzia January 4, 2022 simu zote ambazo zinatumia mfumo huo wa zamani hazitoweza kufanya kazi kwenye sehemu ya Kupiga simu au Phone calls, Sehemu ya SMS au ujumbe mfupi, pamoja na sehemu ya kupiga simu za dharura.
Mbali na hayo, Blackberry pia imetangaza kuwa inawezekana kuwa simu hizo zikakosa uwezo wa kutumia Internet kwa usahihi ikiwa pamoja na apps za Blackberry kama vile BlackBerry Link, BlackBerry Desktop Manager, BlackBerry World, BlackBerry Protect, BlackBerry Messenger, pamoja na BlackBerry Blend.
Kama wewe ni mtumiaji wa simu hizi unaweza kuhakikisha una hamisha data zako mapema kabla ya tarehe 4 ili kuepuka kupoteza data zako kutokana na kushindwa kutumia internet kwenye simu hizo.
Blackberry ilitangaza kuacha kutengeneza simu zenye mfumo wake wa uendeshaji kuanzia mwaka 2015, kabla ya kubadilisha kampuni hiyo kutoka kampuni ya utengenezaji wa vifaa kuwa kampuni ya utengenezaji wa programu.
Natumia simu aina ya Infinix inazima kila mara naombeni msaada tatizo hili lisiwepo tena Asante