Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Simu za Huawei Mate 30 Kuingia Sokoni Bila Soko la Play Store

Bado hakuna taarifa kamili lakini huwenda simu hiyo ikaja bila Play Store
Simu za Huawei Mate 30 Kuingia Sokoni Bila Soko la Play Store Simu za Huawei Mate 30 Kuingia Sokoni Bila Soko la Play Store

Katika kuendelea kwa matokeo ya vita vya kibiashara kati ya kampuni ya Huawei na Serikali ya marekani, hivi karibuni wapenzi wa simu za Huawei huwenda wakashindwa kutumia soko la Play Store kwenye simu mpya za Huawei Mate 30 zinazo tarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka mtandao wa BBC, kampuni ya Huawei imeshindwa kupata vibali maalum ambavyo vinawezesha kampuni hiyo kuendelea kutumia mfumo wa Android na programu zake kama kawaida. Ripoti kutoka mtandao wa Reuters zinadai kuwa, Serikali ya marekani iliruhusu kampuni za marekani kuomba vibali maalum vya kuendelea kufanya biashara na kampuni ya Huawei na tayari hadi sasa kampuni zaidi ya 130 zimetuma maombi ya vibali hivyo.

Advertisement

Hata hivyo inasemekana kuwa kampuni ya Google sio moja ya kampuni hizo 130 ambazo tayari zimeonyesha nia ya kuendelea kufanya biashara na kampuni ya Huawei. Hivi leo kampuni ya Huawei imetengaza kuzindua simu yake mpya ya Huawei Mate 30 tarehe 19 mwezi wa tisa.

Mpaka sasa bado hakuna uhakika kama Huawei inayo mbadala wa soko la Play Store, ukitegemea soko la Play Store linategemewa na watumiaji wengi wa simu za Android kutokana na kuwepo na programu nyingi ikiwa pamoja na Apps maarufu kama YouTube, Gmail, Google na nyingine kama hizo ambazo hazito kuwepo kwenye simu ya Huawei Mate 30 kama kampuni hiyo haitofikia muafaka na kampuni ya Google.

Mbali na hayo Huawei Mate 30 inategemewa kuwa ni simu yenye uwezo mkubwa sana wa kamera, huku kamera zake zikiwa na muundo wa duara kubwa tofauti na simu nyingine zote za Huawei ambazo tayari zimesha zinduliwa hivi karibuni.

Simu za Huawei Mate 30 Kuingia Sokoni Bila Soko la Play Store

Mbali na hayo, inasemekana kuwa Huawei Mate 30 na Mate 30 Pro zinatakuja na processor yenye nguvu ya Kirin 990 chipset ambayo inategemewa kuzinduliwa kwenye mkutano wa IFA utakao fanyika hivi karibuni. Tetesi hizo zinadai kuwa, simu Mate 30 na Mate 30 Pro zote zitakuja na vioo vikubwa vya inch 6.7 huku vikiwa vime tengenezwa kwa teknolojia ya OLED.

Kwa sasa hayo ndio machache ambayo tumefanikiwa kuyasikia kuhusu simu mpya za Huawei Mate 30 na Mate 30 Pro. Kama unataka kujua zaidi basi hakikisha hiyo tarehe 19 unakuwa na sisi kwani tutakujuza yote unayotakiwa kujua kuhusu simu hii, ikiwa pamoja na hilo la soko la Play Store.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use