Hizi Hapa Simu Nzuri za Tecno za Kununua Mwaka 2020

Hizi hapa simu nzuri za TECNO unazoweza kununua kwa sasa
Hizi Hapa Simu Nzuri za Tecno za Kununua Mwaka 2020 Hizi Hapa Simu Nzuri za Tecno za Kununua Mwaka 2020

Mwaka 2020 tayari umefika tarehe 3 mwezi wa pili, na hasi sasa bado kampuni ya Tecno haijazindua simu mpya na bado hakuna tetesi za ujio wa simu mpya kwa mwezi huu. Lakini pamoja na hayo zipo simu nzuri ambazo unaweza kununua kwa sasa ambazo na uhakika zinaweza kukidhi mahitaji yako ya kila siku.

Kuliona hilo leo nimekuletea list hii fupi ya simu nzuri za Tecno ambazo unaweza kuzinunua kwa sasa mwaka huu 2020, simu hizi ni nzuri na zinaweza kuwa bora zaidi kulingana na matumizi yako. Mbali na hayo list hii imehusisha simu za aina zote yani simu za bei rahisi na simu za bei ghali hivyo ni tumaini yangu kuwa utaweza kupata simu nzuri ya kununua kwa sasa.

Advertisement

Basi bila kuendelea kupoteza muda zaidi twende tukangalie list hii, kitu cha msingi kumbuka simu zote kwenye list hii ni bora na hatujapanga list hii kulingana na ubora hivyo ya mwisho ni bora kama ilivyo simu ya kwanza kwenye list hii, baada ya kusema hayo twende moja kwa moja kwenye list hii.

TECNO Pop 2F – Tsh 150,000 hadi Tsh 180,000

Hizi Hapa Simu Nzuri za Tecno za Kununua Mwaka 2020

TECNO Pop 2F ni toleo jipya la simu za bei nafuu za TECNO Pop 2 ambazo zilizinduliwa rasmi mwaka 2018, simu hii inakuja na maboresho kama vile ukubwa wa ndani wa GB 16 tofauti na toleo lililopita ambalo lilikuwa na ukubwa wa ndani wa GB 8. Simu hizi ni kwa sasa zinapatikana kwa bei nafuu sana hapa Tanzania na unaweza kuzipata kwenye maduka mbalimbali hapa Tanzania.

Soma Zaidi >

TECNO Pouvoir 3 – Tsh 350,000 hadi Tsh 400,000

Hizi Hapa Simu Nzuri za Tecno za Kununua Mwaka 2020

TECNO Pouvoir 3 ni simu nyingine kutoka kampuni ya Tecno iliyozinduliwa mwaka 2019, kama unavyojua kuhusu simu hizi kutoka Tecno huwa na uwezo mkubwa sana wa kudumu na chaji. Pamoja na sifa nyingine za simu hii nadhani utafurahia zaidi simu hii kwa upande wa chaji pamoja na ugumu na ubora wa simu hii.

Soma Zaidi > 

TECNO Phantom 9 – Tsh 600,000 hadi Tsh 700,000

Hizi Hapa Simu Nzuri za Tecno za Kununua Mwaka 2020

TECNO Phantom 9, simu hii ni simu yenye sifa bora kuliko simu zote za tecno kwa mwaka huu 2019, mbali na hayo simu hii ni moja ya simu zilizo shikilia rekodi ya kuwa simu za kwanza za kutoka TECNO kuwa na kamera zaidi ya mbili kwa nyuma, pamoja na teknolojia mpya ya kioo cha AMOLED ambacho hakijawahi kutumiwa kwenye simu za TECNO. Unaweza kusoma hapa kujua mambo ambayo ulikuwa huyajui kuhusu simu hii. Kumbuka bei ya simu hii inaweza kubadilika.

Soma Zaidi >

TECNO Camon 12 – Tsh 300,000 hadi Tsh 450,000

Hizi Hapa Simu Nzuri za Tecno za Kununua Mwaka 2020

Camon 12 ni simu nyingine bora ya TECNO iliyozinduliwa mwaka 2019, simu hii inakuja na sifa bora pamoja na muonekano wa kisasa kuliko simu zote za Camon zilizotoka hadi sasa. Simu hizi zinakuja kwa matoleo matatu ya Camon 12, Camon 12 Pro, pamoja na Camon 12 Air zote zikiwa na muonekano unaofanana. Kumbuka bei inaweza kuwa tofauti kulingana na eneo ulilopo.

Soma Zaidi >

TECNO Spark 4 – Tsh 280,000 hadi Tsh 350,000

Hizi Hapa Simu Nzuri za Tecno za Kununua Mwaka 2020

Kampuni ya TECNO imefunga mwaka huu 2019 kwa kuzindua simu mpya ya TECNO Spark 4, simu hii ni toleo la maboresho la simu ya TECNO Spark 3 ambayo ilitoka mwaka 2018, simu hii kama ilivyo Camon 12 nayo inakuja na sifa bora pamoja na muonekano bora. Mbali na hayo simu hii nayo inakuja na matoleo mawili tofauti kama ya Spark 4 na Spark 4 Air, simu zote zinafanana kwa muonekano. Kumbuka bei inaweza kuwa tofauti kulingana na eneo ulilopo.

Soma Zaidi > 

Na hizo ndio simu ambazo kwa sasa ni simu nzuri za kununua kutoka TECNO. Kama unataka kujua simu nyingine nzuri za kununua kwa mwaka huu 2020, basi hakikisha unasoma makala hii hapa nime kuwekea sifa kamili za simu hizo pamoja na bei zake. Kama wewe ni mpenzi wa simu za Infinix basi unaweza kupitia list ya simu za Infinix ambazo unaweza kununua kwa mwaka huu hapa.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use