Najua wewe ni mmoja wa wapenzi wa simu za Infinix na kuliona hili, leo nimeona nije na list ya simu hizi bora za Infinix ambazo najua zinaweza zikawa bora kwa namna moja ama nyingine hii ikiwa inategemeana sana na mahitaji yako binafsi kwenye simu janja.
Kupitia makala hii tutaenda kuangalia simu hizi nzuri za infinix ambazo unaweza kununua kwa mwaka huu 2020, kumbuka simu zote hizi kwa sasa zinapatikana kwenye maduka mbalimbali hapa Tanzania.
Mbali na kuonyesha simu hizi nzuri, pia utaweza kuona bei ya simu hizi ikiwa pamoja na sifa kamili za simu hizi kwa kubofya sehemu iliyo andikwa soma zaidi. Pia kumbuka bei hizi zinaweza kubadilika kutokana na eneo unapo nunua moja kati ya simu hizi. Basi bila kupoteza muda twende tukangalie list hii, kumbuka list hii haijapagwa kwa namba hivyo simu zote kwenye list hii ni bora.
TABLE OF CONTENTS
Infinix Hot 7
Infinix Hot 7 ni toleo bora la simu za infinix, simu hii inakuja na muonekano mzuri pamoja na sifa ambazo zinafanana na thamani ya pesa unayo nunulia simu hii. Mbali ya yote kamera za simu hii ni bora na zenye uwezo wa kuchukua picha nzuri sana ukilinganisha na simu nyingi za infinix ambazo zimetoka miaka iliyopita.
BEI – TZS 260,000 hadi TZS 320,000
Soma Zaidi Kuhusu Infinix Hot 7 >
Infinix Zero 6
Kama kweli wewe ni mpenzi wa simu zenye kamera nzuri basi lazima utakuwa umewahi kusikia simu ya Infinix Zero 6, simu hii inakuja na kamera nzuri sana na pia inakuja na sifa bora zaidi ambazo zinafanana na bei yake. Kifupi ni kuwa, kweli kampuni ya infinix imekuwa ikijitahidi sana kuja na simu zenye ubora pamoja na kamera nzuri kama watu wengi wanavyopenda. Simu hii inakuja kwa matoleo mawili ya Infinix Zero 6 pamoja na Zero 6 Pro.
BEI – TZS 600,000 had TZS 850,000
Soma Zaidi Kuhusu Infinix Zero 6>
Infinix S4
Kwa wale wapenzi wa kamera hasa selfie basi na uhakika tayari wanajua kuhusu infinix S4, simu hii ni toleo la maboresho la infinix S3 ambayo ilitoka mwaka uliopita, simu hii kwa sasa inakuja na sifa nzuri sana pamoja na muonekano wa kisasa hasa kwenye kioo chale kutokana na muundo wake wa water drop notch, simu hii inakuja na kamera zenye nguvu sana huku kamera ya mbele ikiwa na MP 32. Unaweza kupata Infinix S4 kwa matoleo mawili ya S4 na S4 Pro.
BEI – TZS 350,000 hadi TZS 450,000
Soma Zaidi Kuhusu Infinix S4 >
Infinix Smart 3
Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanapenda simu zenye uwezo mzuri lakini kwa bei nafuu basi ni vyema ufahamu simu mpya ya Infinix Smart 3, simu hizi zinakuja na matoleo mawili toleo la Smart 3 pamoja na Smart 3 Plus. Simu hii inakuja na uwezo mzuri wa kudumu na chaji ikiwa pamoja na kupiga picha nzuri sana ambazo unaweza kuzifanya ziwe nzuri zaidi kwa kutumia mfumo wa AI ambao upo ndani ya simu hizo.
BEI – TZS 370,000 hadi TZS 420,000
Soma Zaidi Kuhusu Infinix Smart 3 >
Infinix Note 6
Infinix Note 6 ni moja kati ya simu bora ambazo naweza kusema inashindania na pacha mwenzake TECNO Phantom 9, simu hii inakuja na sifa nzuri pamoja na muonekano wa kisasa huku nayo ikiwa na kioo kizuri na bora cha AMOLED. Mbali na ubora wake kwa upande wa sifa simu hii pia inakuja na kamer nzuri ikiwa pamoja na battery bora yenye uwezo wa kudumu na chaji zaidi.
BEI – TZS 550,000 hadi TZS 670,000
Soma Zaidi Kuhusu Infinix Note 6 >
Infinix Hot 8
Kwa mara nyingine wapenzi wa simu za bei rahisi zenye ubora wanapatiwa toleo jipya la Infinix Hot 8, simu hii ni moja kati ya simu ambazo zinapatikana kwenye list ya simu zinazopendwa zaidi na watumiaji wa Infinix, huku ikiwa inapatikana kwa bei nafuu zaidi. Simu hii inakuja na kamera bora ikiwa na teknolojia ya AI pamoja na uwezo mkubwa sana wa kudumu na chaji kwa muda mrefu.
BEI – TZS 280,000 hadi TZS 380,000
Soma Zaidi Kuhusu Infinix Hot 8 >
Infinix S5
Kampuni ya Infinix imefunga mwaka 2019 kwa kutoa simu mpya ya Infinix S5, simu hii ni moja kati ya simu nzuri sana kwa wapenzi wa picha na pia kwa wale wanaotaka kwenda na wakati. Kama unataka simu yenye muonekano mzuri na yenye sifa bora basi simu hii ndio simu yako kwa sasa. Kupitia simu hii utaweza kupata mfumo mpya wa Android 9 wenye sehemu mpya mbalimbali ikiwa pamoja na sehemu itakayo kuwezesha kupokea simu yako bila kuishika.
BEI – TZS 350,000 had TZS 400,000
Soma Zaidi Kuhusu Infinix S5 >
Na hizo ndio simu nzuri za Infinix unazoweza kununua kwa mwaka huu 2020, kumbuka simu hizi tayari zinapatika kwenye maduka mbalimbali kwa hapa Tanzania. Kama unataka kujua simu nyingine nzuri za infinix unaweza kusoma hapa kujua simu bora za infinix, pia unaweza kusoma hapa ili kujua simu za bei nafuu za infinix ambazo unaweza kuzipata kwa bei rahisi chini ya Shilingi za Tanzania TZS 300,000.
Kama wewe ni mpenzi wa simu za TECNO pia tunayo list ya simu nzuri za TECNO ambazo unaweza kununua kwa sasa mwaka huu 2020, soma hapa kujua list nzima. Kwa habari zaidi kama hizi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.
Simu hizo ni nzuri ila bei kubwa sana vipi ukiwa na 150000 au 180000 huwezi kupata maana mimi nazikubari sanaaaa