Wote tumeshawahi kusikia yale mananeno kuwa simu nzito ndio bora kuwa nayo, lakini ulishajiuliza kwanini.? Wengi wetu hili hatulijui bali tunafuata kile ambacho tumekikuta na ambacho wataalamu wetu wamekua wakituambia. Ili kukusaidia kujua ni simu gani ni nzuri kwako kutumia kati ya simu nzito ama nyepesi ifuatayo ni listi ya faida na hasara za simu nzito pamoja na simu nyepesi.
- Faida za Simu Nyepesi
Watu wengi wamekua wakichukulia simu nyepesi ni mbaya kiasi kwamba hata mtu wakati ana nunua simu huwa kama ana ipima uzito kwa mikono ili kujua kama simu hiyo ni orignal au feki, lakini hapo tunapoteza kabisa maana kwani simu nyepesi maana yake ni kwamba simu hiyo ni ya kisasa zaidi kiasi kwamba vitu vyake vingi vimetengenezwa vikiwa vidogo zaidi.
Simu nyingi za sasa zinatengenezwa zikiwa nyepesi hii ni kutokana na kuja kwa teknolojia mpya ambazo zinawezesha vifaa vya ndani vya simu kutengenezwa vikiwa vidogo na vyenye nguvu zaidi, hali hiyo husababisha simu hiyo kubaki na nafasi ambayo unakuta haina kitu kabisa na ndio maana unakuta simu hiyo ni nyepesi.
Faida nyingine ya simu nyepesi ni pale inapoanguka, simu nyingi nzito zikianguka chini utakuta kioo au kifaa chochote cha nje au ndani ya simu lazima kitaharibika, lakini simu nyepesi huweza kuwa na uwezekano mkubwa wa kupona hata kama ikianguka kutoka umbali mrefu.
Pia simu nyepesi wakati mwingine ina maanisha ni simu ya kisasa kwani hata ukiangalia uzito wa TV ya miaka ya zamani ni tofauti kabisa na TV ya miaka ya sasa, hii ikiwa na maana kuwa uzito wa Samsung Galaxy S4 sio sawa na uzito wa Samsung Galaxy S7 kwani S4 ni nzito kuliko S7.
- Hasara za Simu Nyepesi
Kuna hasara chache za kuwa na simu nyepesi moja wapo ni kuwa, mara nyingi vifaa vya ndani vya simu hizi nyepesi huwa ni ngumu sana kupatikana au mara nyingine huwa na bei ya juu ukitofautisha na vifaa vya simu zile ambazo hua ni nzito.
Hapa nina maana kuwa leo hii ukiulizia kifaa cha simu ya Samsung Galaxy S4 (simu nzito) ni rahisi kukipata kuliko kupata kifaa cha Samsung Galaxy S7 (simu nyepesi) hata bei yake pia hua ni tofauti kabisa mara nyingi kifaa cha Samsung Galaxy S7 ni ghali kuliko kifaa cha Samsung Galaxy S4, na hii sio sababu tu yakuwa simu hiyo ni ya sasa bali hata upatikanaji wake huwa ni mgumu kwa wauzaji wa vifaa hivyo.
- Faida za Simu Nzito
Mara nyingi simu hizi huwa na ugumu flani kwenye kava lake la nje hii inasababishwa na kuwa mara nyingi simu hizi uzito wake hautokani na vitu vya ndani pekee, bali kuna wakati simu hizi huwa na uzito wa kwenye makava kwa mfano simu za iPhone mara nyingi huwa zina makava yaliyotengenezwa na Silicone ambayo hii ni aina flani ya aluminum nzito ambayo ndio hufanya simu hizo kuwa nzito na ngumu.
Faida nyingine ya simu nzito ni kuwa mara nyingi simu hizi huwa na unafuu wa upatikanaji wa vifaa vyake vya ndani kutokana na upatikanaji wake kuwa mrahisi kidogo. Sio simu zote nzito vifaa vyake upatikana kwa urahisi bali simu nyingi nzito huwa hivyo.
- Hasara za Simu Nzito
Nadhani hapa hakuna haja ya maelezo marefu kwani kama umesoma makala hii kutoka mwanzo lazima utakua umejua hasara za kuwa na simu nzito, hasara hizo ni pamoja na simu hizo nyingi huwa ni za siku nyingi, simu hiyo ikianguka kutoka kwenye umbali mrefu uwezekano wa kupona ni mdogo san ukilinganisha na simu nyepesi pamoja na hasara nyingine nilizo zitaja hapo hawali.
Mwisho ni muhimu kukumbuka kufanya uchunguzi kabla na baada ya kununua simu, hii ikiwa ni pamoja na kuangalia uzito wa simu hiyo kwenye sifa za simu unayotaka kununua. Pia kujua uzito wa simu yako hata baada ya kununua ni vizuri kwani utaweza kujua namna ya kutunza simu yako zaidi.
Nimeipenda sanaaaa Yani Imenisaidia kujua zamani nilikua najua simu nzito ndio issue. Doh Thanks Tanzania Tech
Asante Hamisi kwa kutembelea Tanzania Tech, Tunafurahi wewe kujifunza Karibu Sana
Oky Nice blog
Asante Sana Mila
nimeipenda blog hii kwani napata kujua vitu vingi sana
Asante sana Bensonendelea kutembelea kila siku