Kampuni ya Nokia hivi karibuni imezindua simu mpya ya Nokia XR20, simu hii imeshikilia vichwa vya habari hivi karibuni kwa kuwa simu hii ni moja kati ya simu tofauti sana kutoka kampuni ya Nokia.
Simu hii inasemekana kuwa simu ngumu zaidi kuwahi kutengenezwa na kampuni ya Nokia kupita HMD Global ambao kwa sasa ndio waendeshaji wa kampuni ya Nokia.
Simu hii inakuja na sifa za kawaida ambazo zinapatikana kwenye simu nyingi lakini moja ya sababu ya kuandika hapa ni kutokana na simu hii kuwa ngumu zaidi, unaweza kutazama video hapo chini kujua zaidi.
Simu hii kwa sifa inakuja na sifa kama ifuatavyo. Simu hii inakuja na RAM ya GB 6, uhifadhi wa ndani wa GB 128, pamoja na mfumo wa Android 11, mbali ya hayo simu hii inaendeshwa kwa kutumia battery ya Li-Po yenye uwezo wa hadi mAh 4630 yenye teknolojia ya Fast charging.
Kwa upande wa CPU simu hii inakuja na Octa-core (2×2.0 GHz Kryo 460 & 6×1.8 GHz Kryo 460), ambayo imetengenezwa na Chipset ya Qualcomm Snapdragon 480 5G. Pia kwa upande wa game simu hii haipo nyuma kwani utaweza kucheza game za kawaida ambazo zita kuwa zinapewa nguvu na GPU ya Adreno 619.
Mbali na hayo yote ugumu wa simu hii unakuja kwa kuwa simu hii imetengenezwa kuimili mikiki mikiki kupitia teknolojia ya IP68 ambayo huzuia vumbi na maji ya ujazo wa m 1.5 kwa dakika 60. Pia simu hii inakuja na teknolojia ya Drop-to-concrete resistance from up to 1.8 m, pamoja na MIL-STD-810H compliant. Pia kioo cha simu hii kina ulinzi wa Corning Gorilla Glass Victus.
Itoshe tu kusema simu hii ni bora sana kwa mazingira magumu au kwa watu ambao hufanya kazi ngumu sana. Unaweza kusoma zaidi kuhusu Nokia XR20 hapa.