Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kutana na Simu Ndogo Ngumu Kuliko Zote Yenye Uwezo wa 4G

Simu hii inayo fingerprint pamoja na uwezo wa kuzuia maji na vumbi
Atom simu ndogo ngumu Atom simu ndogo ngumu

Ni kweli kwamba kwenye miaka ya karibuni, simu janja zimekuwa zikibadilika sana kwa maumbo, kumekuwa na simu kubwa zenye vioo vikubwa, simu ndogo zenye vioo vidogo lakini pia kumekuwa na simu ndogo sana zenye uwezo wa simu kubwa. Hata hivyo yote haya yanaonyesha mabadiliko ya teknolojia ambayo yanakuja kwa kasi sana hasa kwenye teknolojia nzima ya simu za mkononi.

Kuonyesha hayo, hivi karibuni kampuni moja ya nchini marekani ambayo pia imetengeneza simu ndogo ya Jelly, imetangaza kuja tena na simu nyingine ya Atom, simu hii inasemekana ni ndogo kuliko zote na pia ni simu ngumu zaidi na pia vilevile ni simu ya kwanza ya ukubwa huo kuwa na uwezo wa Fingerprint sensor.

Advertisement

The Atom inakuja na kioo cha inch 2.45-inch, chenye resolution ya 240 x 432 display; Simu hii pia inakuja na RAM ya 4GB, mfumo wa uendeshaji wa Android 8.1 Oreo, Kamera ya nyuma ya Megapixel 16, na kwa mbele inakuja na kamera ya megapixel 8. Mengineyo yanayo patikana kwenye simu hii ni pamoja na Radio FM, Laini mbili, Uwezo wa NFC capability, Sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack, USB Type-C kwa ajili ya kuchaji simu na bila kusahau kwa mbele simu hiyo inakuja na sehemu ya ulinzi ya fingerprint.

Mbali na hayo simu hiyo inakuja na teknolojia ya kuzuia maji na pia inakuja na teknolojia ambayo inafanya simu hiyo kuwa ngumu na imara zaidi. Hata hivyo kwa mujibu wa kampuni hiyo, Atom inakuja na uwezo mzuri zaidi wa kuzuia maji kiasi kwamba unaweza kupiga picha chini ya maji.

Simu hii ikifanikiwa kufika sokoni inatarajiwa kuuzwa kwa dollar za marekani $300 sawa Tsh 683,000. Kwa sasa kampuni inayo tengeneza simu hii bado iko kwenye hatua za awali za kutafuta fedha kwa ajili ya kufikisha simu hii sokoni, unaweza kuchangia kampuni hiyo kupitia tovuti ya Kickstarter.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use