Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Hapa Simu Ngumu Zaidi Hadi Sasa Mwaka (2018)

Kama ulikua hujui hizi hapa ndio simu ngumu kuliko zote mwaka 2018
simu ngumu mwaka 2018 simu ngumu mwaka 2018

Ni kweli kwamba wengi wetu tunatumia smartphone, lakini ni watu wachache sana duniani wenye simu zenye uwezo wa kudumu kwa muda mrefu kwani hata makampuni yanayotengeneza simu hayazipendi simu hizi kwani zinamfanya mtumiaji kubaki na simu moja kwa muda mrefu na hii kufanya mauzo ya simu kupungua.

Lakini pamoja na yote hayo bado zipo simu ambazo zinasemekana kuwa ni simu ngumu zaidi, simu hizi zinasemekana kupitia majaribio mbalimbali ambayo kweli yanafanya simu hizi kuvikwa taji hilo la simu ngumu. Leo hapa Tanzania Tech tutaenda kuangalia simu hizi ambazo kama umekuwa ukiangusha simu kila mara pengine ni wakati wa kuwaza kufikiria kununua moja ya simu hizi, basi bila kupoteza muda twende tukangalia simu hizi.

Advertisement

5Blackview BV9500 Pro

Blackview-BV9500 Pro sio simu ya muda mrefu sana, simu hii imetoka hivi karibuni na ni moja kati ya simu ambazo ukweli ni simu ngumu sana, simu hii inakuja na uwezo wa kuzuia maji au vimiminika vingine. Pia simu hii inauwezo wa kuimili pale inapo kanyagwa na gari. Blackview-BV9500 Pro inakuja na mfumo wa Android 8.0, Kamera mbili za Megapixel 16 zenye uwezo wa kupiga picha hadi chini ya maji.

4. Blackview BV7000 Pro

Blackview BV7000 Pro ni simu nyingine ambayo ni simu ngumu sana, simu hii kama ulivyo ona kwenye video inauwezo wa kupitia mambo mengi bila hata kuharibika au kuzima. Simu hii inakuja na mfumo wa Android 6.0 “Marshmallow” kioo cha inch 5, ukubwa wa ndani wa GB 64 pamoja na RAM ya GB 4, simu hii pia inakuja na uwezo wa kuzuia maji pamoja na uwezo wa kupiga picha kwenye maji kwa kutumia kamera ya nyuma ya Megapixel 13.

3. Ulefone Armor 2

Ulefone Armor 2 ni simu nyingine ambayo ni ngumu kuliko simu nyingine za kawaida simu hii inauwezo wa kuzia maji kwa muda hadi wa dakika 30 pamoja na uwezo wa kuzuia isiharibike hata kwenye sehemu yenye mteremko simu hii ya Ulefone Armor 2 inakuja na mfumo wa Android 7.0  Nougat, kioo cha inch 5, ukubwa wa ndani wa GB 64 pamoja na RAM ya GB 6.

2. Doogee S60

Doogee S60 ni simu nyingine ambayo kweli ni nondo, simu hii inauwezo wa kushinda majaribio kama ya moto, kukanyagwa na gari na mambo mengine mengi simu hii inakuja na mfumo wa Android 7.0 Nougat, kioo cha inch 5.2 ukubwa wa ndani wa GB 64 pamoja na RAM ya GB 6. Simu hii inapiga picha kwenye maji kwa kutumia kamera zake za Megapixel 21 kwa nyuma na kamera ya Megapixel 8 kwa mbele.

1.AGM X2

AGM X2 ni moja kati ya simu ambazo ni simu ngumu sana kwa mwaka 2017 – 2018, simu hii ni ngumu sana na ukweli inaweza kuimili mambo mbalimbali. Kwenye video hapo juu simu ya AGM X2 imeonekana mara nyingi na pia utaona kuna simu nyingine za AGM. Simu ya AGM X2 inakuja na mfumo wa Android 7.0 Nougat, Ukubwa wa ndani wa GB 128, RAM ya GB 6 pamoja na kamera mbili za nyuma zenye uwezo wa Megapixel 12 kila moja. Kwa mbele simu hii inakuja na kamera ya 16.

Na hizo ndio simu ngumu zaidi hadi sasa mwaka huu 2018, simu hizi zimeingia kwenye list hii kutokana na kupitia majaribio ambayo simu nyingine za kawaida haziwezi kupitia. Kama umependa list hii unaweza kusoma hapa kujua list ya laptop ngumu zaidi hadi sasa mwaka 2018.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use