Hapa Tanzania Tech tumeshaona simu ndogo mbalimbali zenye uwezo wa kufanya mambo mbalimbali, lakini ilikuwa bado hatujawahi kuangalia simu ndogo kuliko zote duniani hadi kufikia siku ya leo.
Zanco Tiny T1 ndio simu inayoshikilia rekodi ya dunia kwa kuwa simu ndogo kuliko zote duniani, simu hii haitumii mfumo wa Android wala iOS ila inakuja ikiwa inatumia mtandao wa 2G pamoja na uwezo wa laini ndogo ya simu (Nano Sim), pamoja na uwezo wa kuhifadhi hadi majina 300 kwenye phonebook yake.
Zanco Tiny T1 ina ukubwa wa size ya dole gumbu la mtu mzima na inauwezo wa kupiga simu kupokea simu pamoja na kutuma ujumbe mfupi au SMS. Battery ya simu hii inauwezo wa kudumu na chaji siku tatu huku ikiwa na uwezo wa kukaa hadi dakika 180, kama unaongea na mtu mfululizo. Zanco Tiny T1 inauzwa Euro £39 sawa na shilingi za Tanzania 116,000 kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo.
Simu hii tayari inapatikana huko nchini marekani na baadhi ya masoko ya mtandaoni, hivyo ni rahisi kuweza kuipta kwa kuinunua kupitia masoko hayo.
kazi nzuri
Asante karibu sana.