Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Mkono Wako Unaweza Kuzuia Network Kwenye Simu Yako

Utafiti unaonyesha kuwa kuna uwezekano mkono wako kuadhiri simu yako
Simu mkononi Simu mkononi

Je, unafaa kushikilia simu yako kwa kutumia mkono upi…? Utafiti umebaini kwamba mkono unaweza unaathiri jinsi simu yako inapokea mawimbi yaani Network, Utafiti huo unasema simu tofauti hufanya vizuri ikiwa imeshikiliwa kwa kutumia mkono mmoja kuliko mkono mwingine.

Prof Gert Pedersen, kutoka chuo kikuu cha Aalborg anasema kwamba antena (kifaa kinachopokea mawimbi) za simu huwa zimewekwa mahali ambapo binadamu hushikilia simu yake, na hivyo kuathiri jinsi simu inapokea mawimbi.

Advertisement

Kwa Mfano kwa mkono wa kushoto Miongoni mwa simu zinazofanya vyema zikiwa zimishikiliwa kwa mkono wa Kushoto ni pamoja na  Samsang Galaxy s7 Edge, simu nyingi za Microsoft Lumia pamoja na Huawei P9.

Kwa upande mwingine wa mkono wa kulia, Miongoni mwa simu zinazofanya vyema zikiwa zimishikiliwa kwa mkono wa kulia ni pamoja na iPhone 6S Plus, LG G5, HTC 10. Hata hivyo Prof Gert Pedersen anasema ukitumia simu yako bila kuishika sikioni kuna imarisha upatikanaji wa mawimbi ikilinganishwa na wakati ambapo umeishikilia.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.

Chanzo : BBC Swahili

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use