Kama kawaida bado mkutano MWC 2018 au Mobile World Congress unaendelea kufanyika huko nchini Barcelona, Siku ya leo moja kati ya habari kubwa ni uzinduzi wa matoleo mapya ya simu za ZTE, simu hizi mpya za ZTE Blade V9 pamoja na ZTE V9 Vita sasa zinakuja na maboresho na sifa bora zaidi.
Mbali na kuja na sifa bora simu hii inakuja na mfumo wa AI ambao unaweza kutumia kwa kutumia kamera ya simu yako, sifa zingine za simu hizi ni pamoja na –
Sifa za ZTE Blade V9
- Ukubwa wa Kioo – 5.7-inch 2,160×1,080 18:9 display
- Uwezo wa Processor – Qualcomm Snapdragon 450 Octa-core 1.8 GHz processor
- Mfumo wa Uendeshaji – Android Oreo 8.1
- Uwezo wa Kamera – Kamera za nyuma zipo mbili moja ina megapixel 16 na nyingine ina megapixel 5, Kamera ya mbele megapixel 8.
- Uwezo wa Battery – 3100 mAh battery
- Ukubwa wa RAM – GB 3 au GB 4
- Ukubwa wa Ndani – GB 32 au GB 64 inayo ongezwa kwa Micro SD card slot
- Aina ya Ulinzi – Fingerprint reader
- Mengineyo – Headphone jack, Micro USB charging
Sifa za ZTE Blade V9 Vita
- Ukubwa wa Kioo – 5.45-inch 2,160×1,080 18:9 display
- Uwezo wa Processor – Qualcomm Snapdragon 435 Octa-core 1.4 GHz
- Mfumo wa Uendeshaji – Android Oreo 8.1
- Uwezo wa Kamera – Kamera za nyuma zipo mbili moja ina megapixel 13 na nyingine ina megapixel 2, Kamera ya mbele megapixel 5
- Uwezo wa Battery – 3200 mAh battery
- Ukubwa wa RAM – GB 2 au GB 3
- Ukubwa wa Ndani – GB 16 au GB 32 inayo ongezwa kwa Micro SD card slot
- Aina ya Ulinzi – Fingerprint reader
- Mengineyo – Headphone jack, Micro USB charging
Kuhusu bei simu ya ZTE Blade V9 Vita ambayo ndio ndogo kisifa inategemewa kuuzwa kwa dollar za marekani $220 ambayo ni sawa na Tsh 496,089. Wakati simu ya ZTE Blade V9 inategemewa kuuzwa kwa dollar za marekani $330 ambayo ni sawa na Tsh 744,133.50 kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo.
Mimi binafisi hizi nimezipenda Sana Lakini spea ya hizi simu kuzipata ni shda Sana tunaomba msaada