Ni kweli kwamba kampuni ya Tecno ni moja kati ya kampuni inayo ongoza kwa kuuza simu za bei nafuu hapa Afrika, lakini pia kadri siku zinavyokwenda kampuni hii inazidi ongeza ubora wa simu zake ikiwa pamoja na kubadilisha muonekano wa simu zake kwa kiwango kikubwa.
Kama ukingalia list ya simu za tecno zilizotoka mwaka 2018, utaweza kuona simu hizo zina utofauti mkubwa sana kwa upande wa maonekano na sifa za ndani za simu za Tecno zilizotoka mwaka 2019. Hii inaonyesha kuwa kampuni hiyo inaboresha bidhaa zake kwa kasi sana hivyo pengine mwaka 2020 tegemea kuona simu za tofauti kutoka sana kutoka kampuni ya Tecno.
Sasa baada ya kusema hayo hebu sasa tukangalie simu zote za tecno ambazo zimezinduliwa kwa mwaka huu 2019, kumbuka unaweza kupata maelezo zaidi ya simu husika kwa kubofya jina la simu husika.
TABLE OF CONTENTS
TECNO Pop 2F – May 2019
TECNO Pop 2F ni toleo jipya la simu za bei nafuu za TECNO Pop 2 ambazo zilizinduliwa rasmi mwaka 2018, simu hii inakuja na maboresho kama vile ukubwa wa ndani wa GB 16 tofauti na toleo lililopita ambalo lilikuwa na ukubwa wa ndani wa GB 8. Simu hizi ni kwa sasa zinapatikana kwa bei nafuu sana hapa Tanzania na unaweza kuipata kwa kuanzia Tsh 150,000 hadi Tsh 180,000. Kumbuka bei hiyo inaweza kubadilika.
TECNO Pouvoir 3 – June 2019
TECNO Pouvoir 3 ni simu nyingine kutoka kampuni ya Tecno iliyozinduliwa mwaka 2019, kama unavyojua kuhusu simu hizi kutoka Tecno huwa na uwezo mkubwa sana wa kudumu na chaji. Pamoja na sifa nyingine za simu hii nadhani utafurahia zaidi simu hii kwa upande wa chaji pamoja na ugumu na ubora wa simu hii. Kwa sasa TECNO Pouvoir 3 inapatikana hapa Tanzania kwa bei kuanzia Tsh 350,000 hadi Tsh 400,000, kumbuka bei hizi zinaweza kubadilika.
TECNO Phantom 9 – July 2019
TECNO Phantom 9, simu hii ni simu yenye sifa bora kuliko simu zote za tecno kwa mwaka huu 2019, mbali na hayo simu hii ni moja ya simu zilizo shikilia rekodi ya kuwa simu za kwanza za kutoka TECNO kuwa na kamera zaidi ya mbili kwa nyuma, pamoja na teknolojia mpya ya kioo cha AMOLED ambacho hakijawahi kutumiwa kwenye simu za TECNO. Unaweza kusoma hapa kujua mambo ambayo ulikuwa huyajui kuhusu simu hii, hata hivyo Phantom 9 inapatikana kwa hapa Tanzania kwa bei kuanzia Tsh 600,000 hadi Tsh 700,000. Kumbuka bein hii inaweza kubadilika.
TECNO Camon 12 – August 2019
Camon 12 ni simu nyingine bora ya TECNO iliyozinduliwa mwaka 2019, simu hii inakuja na sifa bora pamoja na muonekano wa kisasa kuliko simu zote za Camon zilizotoka hadi sasa. Simu hizi zinakuja kwa matoleo matatu ya Camon 12, Camon 12 Pro, pamoja na Camon 12 Air zote zikiwa na muonekano unaofanana. Simu hizi zinapatikana hapa Tanzania kwa bei kuanzia Tsh 300,000 hadi Tsh 450,000. Kumbuka bei inaweza kuwa tofauti kulingana na eneo ulilopo.
TECNO Spark 4 – September 2019
Kampuni ya TECNO imefunga mwaka huu 2019 kwa kuzindua simu mpya ya TECNO Spark 4, simu hii ni toleo la maboresho la simu ya TECNO Spark 3 ambayo ilitoka mwaka 2018, simu hii kama ilivyo Camon 12 nayo inakuja na sifa bora pamoja na muonekano bora. Mbali na hayo simu hii nayo inakuja na matoleo mawili tofauti kama ya Spark 4 na Spark 4 Air, simu zote zinafanana kwa muonekano. TECNO Spark 4 Inapatikana kwa hapa Tanzania kuanzia shilingi za kitanzania Tsh 280,000 hadi Tsh 350,000. Kumbuka bei inaweza kuwa tofauti kulingana na eneo ulilopo.
Na hizo ndio simu ambazo zimezinduliwa kwa mwaka huu na kampuni ya TECNO, hadi sasa hakuna taarifa zaidi za simu nyingine mpya ya tecno inayotegemea kuzinduliwa siku ndani ya mwaka huu 2019, nadhini hadi mwaka mwingine mungu akipenda tutaenda kuangalia matoleo mpya ya simu za TECNO zitakazotoka mwaka 2020.
Hi, naomba utuandalie maada kuhusu kioo cha AMOLED, utujuze umuhimu wke na faida zke.