Takribani wiki tatu sasa kumekuwa na taarifa mbalimbali kuhusu ujio wa simu mpya za Samsung Galaxy S21 ambazo zinategemewa kuja mapema kuliko ilivyo zoeleka.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, simu za Galaxy S21, S21+, na S21 Ultra zinatarajiwa kuja mwanzoni kabisa wa mwaka 2021, ikiwa ni siku 14 baada ya mwaka mpya. Simu hizo zinatarajiwa kuja na mabadiliko ya muonekano, huku asilimia kubwa ya mabadiliko hayo ikiwa ni kwenye toleo la Galaxy S21 Ultra.
Hadi sasa tayari baadhi ya sifa za simu hii zinajulikana mtandaoni, huku simu ya Galaxy S21 Ultra ikitarajiwa kuja na uwezo zaidi pamoja na uwezo wa kutumia kalamu maarufu kama S-Pen. Hata kuja kwa kalamu ya S-Pen kwenye simu za Galaxy S21 kunasemekana kuwa ni hatua ya Samsung kusitisha toleo la Galaxy Note kwa mwaka 2021.
Mbali na hayo, hivi karibuni imevuja video ya muda mfupi ambayo inasemekana kuwa ndio video yenye muonekano halisi wa Galaxy S21 na Galaxy S21 Ultra.
Kama unavyoweza kuona kwenye video hapo juu, inaonekana kampuni ya Samsung imefanya mabadiliko kwenye muonekano wa kamera za simu hizo huku sasa zikiwa pia zinapatikana kwa muundo mwingine kabisa.
Bila shaka kampuni ya Samsung inataka kutengeneza utambulisho wake kama ilivyo simu mpya iPhone, ambazo zinatambulika sana kwa muonekano wake wa lensi kubwa za kamera zinazopatikana nyuma ya simu hizo.
Kwa sasa baadhi ya sifa za Samsung Galaxy S21, S21 Plus na S21 Ultra ni pamoja na
Samsung Galaxy S21 5G
- Uwezo wa Kioo – Dynamic AMOLED, Inch 6.3
- Uhifadhi wa ndani (ROM) – GB 128 GB na GB 256
- Uwezo wa RAM – GB 8 na GB 12
- Kamera za Nyuma – Kamera tatu 12 MP, 64 MP, 12 MP yenye uwezo wa 8K
- Kamera za Mbele – 10 MP yenye uwezo wa 4K
- Uwezo wa Battery – 4500mAh yenye uwezo wa Fast charging hadi 25W, pia inayo wireless charging.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G, 4G na 5G
Samsung Galaxy S21 Plus 5G
- Uwezo wa Kioo – Dynamic AMOLED, Inch 6.7
- Uhifadhi wa ndani (ROM) – GB 128 GB, GB 256 na GB 512
- Uwezo wa RAM – GB 12
- Kamera za Nyuma – Kamera tatu 12 MP, 64 MP, 12 MP yenye uwezo wa 8K
- Kamera za Mbele – 10 MP yenye uwezo wa 4K
- Uwezo wa Battery – 4800mAh yenye uwezo wa Fast charging hadi 25W, pia inayo wireless charging.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G, 4G na 5G
Samsung Galaxy S21 Ultra 5G
- Uwezo wa Kioo – Dynamic AMOLED, Inch 6.8
- Uhifadhi wa ndani (ROM) – GB 128 GB na GB 512
- Uwezo wa RAM – GB 12 na GB 16
- Kamera za Nyuma – Kamera nne 108 MP, 10 MP, 10 MP, 12 MP yenye uwezo wa 8K
- Kamera za Mbele – 40 MP yenye uwezo wa 4K
- Uwezo wa Battery – 5000mAh yenye uwezo wa Fast charging hadi 25W, pia inayo wireless charging.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G, 4G na 5G
Kwa sasa hizo ndio baadhi ya sifa za Galaxy S21, S21+ na S21 Ultra ambazo zinafahamika, kumbuka sifa hizi zinaweza kubadilika pale Samsung itakapo zindua rasmi simu hizi hapo tarehe 12 January 2021. Kujua sifa kamili, pamoja na bei ya simu hizi pindi zitakapotoka hakikisha unatembelea tovuti yetu ya priceintanzania.