Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Samsung Yazindua Simu Mpya za Galaxy S20 FE (Fan edition)

Simu hizi zinakuja kwa matoleo mawili ya Galaxy S20 FE 4G na Galaxy S20 FE 5G
Samsung Yazindua Simu Mpya za Galaxy S20 FE (Fan edition) Samsung Yazindua Simu Mpya za Galaxy S20 FE (Fan edition)

Kampuni ya Samsung hivi leo imetambulisha matoleo mapya ya simu za Galaxy S20, simu hizi mpya za Galaxy 20 FE 4G na S20 FE 5G zinakuja zikiwa zimechanganya baadhi ya sifa kutoka Galaxy S20 na Galaxy S20 Ultra.

Advertisement

Kwa upande wa kioo, Galaxy 20 FE inakuja na kioo chenye inch 6.5 huku kikiwa kimetengenezwa kwa teknolojia ya AMOLED Display, mbali ya hayo kioo kinakuja na resolution ya hadi pixel 1080 kwa 2400. Kwenye kioo hicho kwa juu kunayo kamera ya selfie yenye uwezo wa Megapixel 32 huku ikiwa na uwezo wa kuchukua video za hadi 4K.

Kwa nyumba Galaxy S20 FE inakuja na kamera tatu, huku kamera kuu ikiwa inakuja na uwezo wa Megapixel 12 na nyingine mbili zikiwa na Megapixel 12 na Megapixel 8. Kamera zote hizo kwa pamoja zinakuja na uwezo wa kuchukua video za hadi 8K.

Samsung Yazindua Simu Mpya za Galaxy S20 FE (Fan edition)

Samsung Galaxy S20 FE inakuja ikiwa imetengenezwa kwa sifa zinazo fanan kidogo na Galaxy S20, huku simu hii ikiwa inakuja kwa matoleo mawili ambayo yanafanana kiasi fulani. Galaxy S20 FE ambayo inayo uwezo wa 5G na Galaxy S20 FE yenye uwezo wa 4G.

Sifa za Ndani za Galaxy S20 FE na S20 FE 5G

Simu zote zinakuja na sifa za ndani zinazo tofautina kidogo, ambapo Galaxy S20 FE 4G inakuja na processor ya Exynos 990 (7 nm+), wakati Galaxy S20 FE 5G yenyewe inakuja na processor ya Qualcomm SM8250 Snapdragon 865 (7 nm+).

Mbali na hayo pia uwezo wa CPU unatofautina huku S20 FE yenye 4G inakuja na CPU ya Octa-core (2×2.73 GHz Mongoose M5 & 2×2.50 GHz Cortex-A76 & 4×2.0 GHz Cortex-A55). Wakati S20 FE 5G inakuja na CPU ya Octa-core (1×2.84 GHz Kryo 585 & 3×2.42 GHz Kryo 585 & 4×1.80 GHz Kryo 585).

Samsung Yazindua Simu Mpya za Galaxy S20 FE (Fan edition)

Kwa upande wa RAM simu zote zinakuja na RAM inayofanana ambayo ni GB 6 huku ikiwa inasaidiwa na uhifadhi wa ndani unaofanana, ROM ya GB 128 au GB 256. Unaweza kuongeza uhifadhi kwa kutumia Micro SD card ya hadi TB 1.

Kwa upande wa battery, Galaxy S20 FE 4G na Galaxy 20 FE 5G zote zinakuja na aina moja ya battery yenye uwezo wa hadi 4500 mAh. Simu hizi pia zinakuja na uwezo wa teknolojia ya Fast Charging yenye uwezo wa hadi 15W, pia simu hii inakuja na teknolojia ya Reverse wireless charging yenye uwezo wa hadi 4.5W.

Samsung Yazindua Simu Mpya za Galaxy S20 FE (Fan edition)

Sifa na Bei Kamili ya Galaxy S20 FE 4G na S20 FE 5G

Simu hizi zinasemekana kupatikana kuanzia siku ya leo kwa pre-order, ambapo simu zote zinatarajiwa kuwafikia wateja mwezi ujao. Kwa hapa Tanzania, tegemea kuona simu hii kwenye maduka mbalimbali kuanzia mwezi wa 10 mwishoni.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use