Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Samsung Yazindua Simu Mpya za Galaxy J7 Max na J7 Pro

Kampuni ya Samsung Yaongeza idadi ya Simu zake kwa kuzindua simu mpya
Galaxy-j7-max Galaxy-j7-max

Kwa wale wapenzi wa simu za samsung basi ni habari njema kujua kuwa kampuni ya samsung imeongeza idadi ya simu zake hivi karibuni kwa kuzindua simu zake mpya za samsung galaxy J7 Max pamoja na Samsung Galaxy J7 Pro.

Simu Hizo mbili zimezinduliwa kwenye mkutano maalum uliofanyika huko nchini india na simu hizo zimezinduliwa zikiwa na huduma za Samsung Pay huduma ambayo kwa bahati mbaya kwa hapa Tanzania bado hatuna. Kikubwa simu hizi zinakuja na sifa bomba zifuatazo.

Advertisement

Kwa upande wa Galaxy J7 Pro simu hii inakuja na kioo cha inch 5.5 ikiwa na teknolojia ya Full HD, simu hii pia itakuja na uwezo wa processor ya Exynos 7870 chipset yenye uwezo wa 1.6 GHz huku ikisaidiwa na RAM ya GB 3. Kwa upande wa ukubwa wa ndani simu hii ina ukubwa wa ndani wa GB 64 na unaweza kutumia memory card kuongeza ukubwa huo, mwisho kabisa simu hii ya Galaxy J7 pro inakuja na battery yenye uwezo wa 3,600 mAh pamoja na sehemu ya fingerprint sensor bila kusahau simu hii inakuja na kamera za kutisha.. za mbele na nyuma zote zikiwa na uwezo wa mmoja wa Megapixel 13 ikiwa na flash nyuma na mbele..Tecno mko wap..?

Kwa upande wa simu mpya Galaxy J Max kama lilivyo jina lake simu hii inakuja na kioo kikubwa cha inch 5.7 uku nayo ikiwa na teknolojia ya Full HD, simu hii itakuja na processor ya MediaTek Helio P20 octa-core processor yenye uwezo wa 1.6 GHz. Kwa upande wa ukubwa wa ndani simu hii itakuja na ukubwa tofauti kidogo japo kuwa hii ndio kubwa simu hii itakuja na ukubwa wa GB 32 uku ikiwa na RAM ya GB 4, sijajua kwanini simu hii imekua na ukubwa mdogo lakini what the hell… kuna memory card unaweza kutumia kuongeza ukubwa wa memory ya simu yako. Mwisho simu hii inakuja na battery sawa na Galaxy J7 pro ambayo ni 3,300 mAh, kama bado unajiuliza kamera simu hizi zote mbili zitafanana kwa hilo kwani zitakuja na kamera ya mbele na yanyuma zote zikiwa na uwezo wa Megapixel 13 pamoja na flash kwenye kamera zote ya mbele na nyuma.

Simu zote hizi zitakuja na toleo jipya kabisa la Android 7 Nougat na simu hizi zinategemewa kuanza kuuzwa nchini india kuanzia June 20 na zitauzwa kwa Rupee INR 17,900 kwa Samsung Galaxy J7 Max sawa na shilingi za kitanzania Tsh 623,262.66 bila kodi na kwa upande wa Samsung Galaxy J7 Pro simu hii itanza kuuzwa kuanzia katikati ya mwezi july na itauzwa kwa Rupee za india INR 20,900 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 727,720.08 bila kodi, kumbuka viwango hivyo ni kutokana na viwango vya kubadili fedha vya leo tarehe 15.06.2017.

Kwa habari zaidi za teknolojia unaweza kuendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku, kumbuka pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote kwa haraka zaidi, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use