Mkutano wa MWC 2018 au Mobile World Congress umeanza rasmi leo huko nchini Barcelona, Huku kampuni mbalimbali za simu nazo zikiwa zipo tayari kuonyesha teknolojia mpya ya simu janja zitakao anza na kuwakilisha mwaka huu 2018.
Wakati tukiwa tunasubiri event kubwa kuliko zote ya uzinduzi wa Samsung Galaxy S9, tayari kampuni zingine zimefanya uzinduzi wa simu zake mpya ambazo zitaufungua mwaka 2018. Kampuni ya Alcatel ni moja kati ya kampuni hizo na kwa mwaka huu Alcatel imezindua simu zake mpya tano pamoja na tablet mbili zenye mfumo wa Android Oreo.
ALCATEL 5
Ikiwa ndio simu ya bei ghali kuliko zote, Alcatel 5 inakuja na kioo cha inch 5.7 chenye resolution ya 1440 x 720 huku ikiwa na inaendeshwa na processor ya octa-core MediaTek pamoja na mfumo wa uendeshaji wa Android Nougat 7.0. Simu hii pia inakuja na teknolojia ya kutambua uso au face recognition huku kwa upande wa kamera ikiwa na kamera moja tu kwa nyuma. Simu hii inategemewa kuuzwa kwa €229.99 sawa na Tsh 640,000.
ALCATEL 3, ALCATEL 3X, na ALCATEL 3V
Hizi ni simu ambazo ni mapacha ambazo zina fanana kwenye sura pamoja na sifa lakini zina tofautiana ukubwa tofauti. Simu ya Alcatel 3 inakuja na kioo cha inch 5.5 na resolution ya 1440 x 720 display, wakati Alcatel 3X inakuja na kioo cha inch 5.7 na resulution ya 1440 x 720 display, huku pia Alcatel 3V ikiwa na kioo cha inch 6 chenye resolution ya 2K display. Simu zote hizi zinatumia processor ya quad-core MediaTek huku zikiwa na teknolojia ya kutambua uso au facial recognition.
Kwa upande wa kamera simu za Alcatel 3X na Alcatel 3V zote zinakuja na kamera mbili kwa nyuma wakati simu ya Alcatel 3 ikiwa inakuja na kamera moja, Vilevile simu za Alcatel 3 na Alcatel 3V zinakuja na mfumo mpya wa uendeshaji wa Android Oreo huku simu ya Alcatel 3X yenyewe inakuja na mfumo wa Android Nougat 7.0. Simu hizi zinakuja kwa bei ya €150 sawa na Tsh 420,000 kwa Alcatel 3, €180 sawa na Tsh 500,000 kwa Alcatel 3X na €190 sawa na Tsh 530,000 kwa Alcatel 3V.
ALCATEL 1X
Alcatel X1 ni moja kati ya simu za bei rahisi na ni moja kati ya simu ambazo zinatumia mfumo wa uendeshaji wa Android Go ambao hutumika kwenye simu zenye uwezo mdogo, simu hii mpya ya Alcatel X1 inakuja na mfumo wa kutambua uso huku ikiwa inauzwa kwa €100 ambayo ni sawa na Tsh 280,000.
TABLET ZA ALCATEL 1T 7 NA ALCATEL 1T 10
Alcatel 1T 7 pamoja na Alcatel 1T 10 ni teblet mpya ambazo zinakuja na mfumo mpya wa uendeshaji wa Android Oreo 8.1 pamoja na processor za quad-core MediaTek ambazo zinasaidiwa na RAM yenye ukubwa wa GB 1. Tofauti ya tablet hizo ni Alcatel 17 7 ina kioo cha inch 7 chenye resolution ya 1024 x 600 display wakati Alcatel 1T 10 inayo kioo cha inch 10 chenye resolution ya 1280 x 800 display. Tablet hizi zitauzwa kwa €70 ambayo ni sawa na Tsh 30,000 kwa Tablet ya Alcatel 1T7 na €100 ambayo ni sawa na Tsh 290,000 kwa tablet ya Alcatel 1T 10.
Simu hizo ambazo ni Alcatel 5, Alcatel 3, 3X, na 3V, pamoja na Tablet za Alcatel 1T 7 na Alcatel 1T zote zinatarajiwa kuingia sokoni kuanzia mwezi wa Nne mwaka huu 2018.
Maoni*kwaihiy alcatel 7 tsh ngapi?
Nilikua naomba kufaham bei yasim hizo za Alcatel