Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kampuni ya TECNO Yazindua Simu Mpya ya Spark 6

TECNO Spark 6 inakuja na kioo kikubwa zaidi pamoja na RAM zaidi
Kampuni ya TECNO Yazindua Simu Mpya ya Spark 6 Kampuni ya TECNO Yazindua Simu Mpya ya Spark 6

Kampuni ya TECNO hivi karibuni imetangaza ujio wa simu yake mpya ya bei rahisi ya TECNO Spark 6, simu hii ni muendelezo wa toleo la TECNO Spark 5 iliyo zinduliwa mapema mwaka huu 2020. Simu hii mpya ya Spark 6 inakuja na maboresho kadhaa huku ikiwa na kioo kikubwa zaidi.

Advertisement

Kwa upande wa kioo hicho, TECNO Spark 6 inakuja na kioo cha inch 6.8 huku kioo hicho kikiwa kimetengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD, ambacho pia kinakuja na uwezo wa kuonyesha picha na video zenye resolution ya hadi pixel 720 kwa 1640.

Kampuni ya TECNO Yazindua Simu Mpya ya Spark 6

Kama ilivyo toleo la TECNO Spark 5, pia toleo la Spark 6 linakuja na kamera ya mbele yenye Megapixel 8 huku ikiwa na uwezo wa kuchukua video za hadi 1080p. Kwa nyuma, Spark 6 inakuja na kamera nne huku kamera kuu ikiwa na Megapixel 16 na nyingine mbili zikiwa na uwezo wa Megapixel 2 kila moja na kamera nyingine ya mwisho ikiwa ni QVGA.

Kampuni ya TECNO Yazindua Simu Mpya ya Spark 6

Kwa upande wa sifa za ndani, TECNO Spark 6 inakuja na RAM ya GB 4, uhifadhi wa ndani yaani ROM ya hadi GB 64, huku ukiwa na uwezo wa kuongeza uhifadhi huo kwa kutumia memory card.

Simu hii inatumia mfumo wa android 10 huku juu yake kukiwa na mfumo wa TECNO HiOS 7.0. TECNO Spark 6 inakuja na Radio FM, sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack, pamoja na sehemu ya ulinzi ya fingerprint ambayo inapatikana kwa nyuma ya simu hiyo.

Kampuni ya TECNO Yazindua Simu Mpya ya Spark 6

Kwa upande wa battery, Spark 6 inakuja na battery kama ya Spark 5, ambayo ni 5000 mAh battery yenye uwezo wa teknolojia ya Fast Charging ya hadi 18W.

Bei ya TECNO Spark 6

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use