Oppo Yazindua Simu Mpya za Reno 4 na Reno 4 Pro

Sifa za Simu mpya za Oppo Reno 4 5G pamoja na Oppo Reno 4 Pro 5G
Oppo Yazindua Simu Mpya za Reno 4 na Reno 4 Pro Oppo Yazindua Simu Mpya za Reno 4 na Reno 4 Pro

Kampuni ya Oppo hivi leo imetangaza ujio wa simu zake mpya za Oppo Reno 4 na Oppo Reno 4 Pro, zote zikiwa ni simu za kwanza za daraja la kati kutoka kampuni ya Oppo kuwa na uwezo wa mtandao wa 5G.

Oppo Yazindua Simu Mpya za Reno 4 na Reno 4 Pro

Advertisement

Oppo Reno 4 Pro

Tukianza na Oppo Reno 4 Pro, simu hii inakuja na kioo cha inch 6.55 kioo ambacho kime tengenezwa kwa teknolojia ya AMOLED huku kikiwa na uwezo wa kuonyesha picha na video zenye resolution ya hadi pixel 1080 kwa 2400.

Mbali na hayo, kioo hicho pia kimetengezwa kwa kutumia Glass ngumu ambayo inafanya kioo hicho kupewa alama ya Corning Gorilla Glass 6. Hata hivyo, kioo hicho pia kinakuja na teknolojia nyingine kama HDR10+, 90Hz refresh rate pamoja nan500 nits, vyote vikiwa vinasaidia kioo hicho kuwa na mwanga bora na uwezo wa kuonyesha vizuri zaidi.

Oppo Yazindua Simu Mpya za Reno 4 na Reno 4 Pro

Tukiwa bado kwa mbele, Oppo Reno 4 Pro inakuja na kamera moja ya selfie yenye uwezo wa Megapixel 32 huku ikiwa na uwezo wa kuchukua video za hadi pixel 1080p@30fps, gyro-EIS. Kamera hiyo pia inasaidiwa na teknolojia ya HDR ili kuchukua picha na video zenye ubora.

Kwa nyuma Oppo Reno 4 inakuja na kamera tatu huku kamera kuu ikiwa na Megapixel 48 na nyingine mbili zikiwa na Megapixel 13 na Megapixel 12. Kamera zote kwa ujumla zinakuja na uwezo wa kuchukua video za hadi 4K@30fps, 1080p@30/60/120fps; gyro-EIS, OIS, HDR.

Oppo Yazindua Simu Mpya za Reno 4 na Reno 4 Pro

Kwa upande wa sifa za ndani, Oppo Reno 4 Pro inakuja na processor ya Qualcomm Snapdragon 765G, processor ambayo ina speed ya CPU ya hadi Octa-core (1×2.4 GHz Kryo 475 Prime & 1×2.2 GHz Kryo 475 Gold & 6×1.8 GHz Kryo 475 Silver). Mbali na hayo simu hii inakuja na uhifadhi wa ndani wa hadi GB 256, huku kukiwa na toleo la ziada lenye uhifadhi wa hadi GB 128.

Mbali na hayo, Oppo Reno 4 Pro inakuja na uwezo wa RAM ya hadi GB 8 huku kukiwa na toleo lingine la ziada lenye RAM ya hadi GB 12. Simu hii pia inakuja na uwezo wa battery ya hadi 4000 mAh battery, huku battery hiyo ikiwa na teknolojia ya Fast Charging ya hadi 65 W, yenye uwezo wa kujaza simu hii hadi asilimia 60% kwa dakika 15, na aslimia 100% kwa dakika 36.

Soma Hapa Kujua Bei ya Oppo Reno 4 Pro kwa Tanzania

Oppo Reno 4

Kwa upande wa Oppo Reno 4, simu hii inakuja na sifa zinazo karibiana na Oppo Reno 4 Pro isipokuwa kioo cha Reno 4 ni kidogo zaidi kikiwa kinakuja na Inch 6.43, huku kwa mbele simu hiyo ikiwa na kamera mbili za Megapixel 32 na Megapixel 2, huku zikiwa na uwezo wa kuchukua video za hadi pixel 1080p@30fps, gyro-EIS.

Oppo Yazindua Simu Mpya za Reno 4 na Reno 4 Pro

Kwa nyuma Oppo Reno 4 inakuja na kamera tatu zenye uwezo wa hadi Megapixel 48 kwa kamera kuu, na Megapixel 8 pamoja na Megapixel 2.Kamera zote kwa pamoja zinakuja na uwezo wa kuchukua video za hadi 4K@30fps, 1080p@30/60/120fps; gyro-EIS, OIS, HDR. Sifa nyingine za Oppo Reno 4 na Oppo Reno 4 Pro zinafanana kwa asilimia 100.

Soma Hapa Kujua Bei ya Oppo Reno 4 kwa Tanzania

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use