Kampuni ya Nokia Kuzindua Leo Simu Mpya ya Nokia 8.1

Jiandae na simu nyingine mpya tatu kutoka kampuni ya Nokia
Kampuni ya Nokia Kuja na Nokia 8.1 Kampuni ya Nokia Kuja na Nokia 8.1

Kampuni ya Nokia ambayo inasimamiwa na kampuni ya HMD Global, hivi leo inatarajia kuja na simu zake mpya za Nokia 8.1, Nokia 3.1 Plus na Nokia 5.1 Plus. Simu hizi mpya zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi huko nchini Dubai huku Nokia 3.1 Plus na Nokia 5.1 Plus zikitarajiwa kwaajili ya soko la ulaya na Nokia 8.1 kwaajili ya soko la dunia nzima.

Kwa mujibu wa tetesi mbalimbali zilizopo mtandaoni, inasemekana kuwa Nokia 8.1 ambayo ndio itakuwa simu ya muhimu kwenye uzinduzi huo, inatarajiwa kuja na sifa zilezile kama zilizopo kwenye simu mpya ya Nokia X7 ambayo ilizinduliwa hivi karibuni kwaajili ya soko la nchini China. Mbali na hayo hivi leo video yenye kuonyesha muonekano unaodhaniwa ni wa Nokia 8.1 imevuja rasmi huku ikionyesha baadhi ya sifa zinazotarajiwa kuja kwenye simu hiyo.

Advertisement

Kwa mujibu wa video hiyo, inaonekana kuwa Nokia 8.1 inatarajiwa kuja na kioo chenye teknolojia ya HDR10 pamoja na kamera mbili za nyuma ambazo hizi ni Zeiss optics ambazo zinakuja na OIS. Mbali na hayo inaonekana kuwa simu hii itakuja na teknolojia ya AI kwenye kamera zake pamoja na sehemu mpya ya beautiful bokeh.

Anyway kifupi ni kwamba inaonekana uzinduzi wa simu hii ya Nokia 8.1 utakuwa ukiangalia zaidi kamera kuliko sifa za simu hiyo. Speaking of Specification, Nokia 8.1 inatarajiwa kuja na Android 9.0 (Pie) RAM ya GB 4 au GB 6, ukubwa wa ndani wa kuchagua kati ya GB 64 na GB 128. Kuhusu processor bado haijajulikana ila endelea kutembelea Tanzania Tech utaweza kujua yote kuhusu simu hii mpya ya Nokia 8.1 ikiwa pamoja na bei yake itakavyokuwa kwa hapa Afrika Mashariki.

Hatimaye kampuni ya Nokia kupitia kampuni ya HMD Global imezindua rasmi simu mpya ya Nokia 8.1, Soma hapa kuweza kujua sifa kamili pamoja na Bei ya simu hii.

Makala imeongezwa tarehe 06/12/2018 kuonyesha tayari uzinduzi wa simu hii umeshafanyka rasmi na sifa kamili pamoja na bei ya simu hii sasa zinafahamika.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use