Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jiandae na Simu Mpya ya Infinix Hot 9 Tarehe 23 Machi 2020

Baada ya Infinix S5 Pro sasa jiandae na simu mpya ya Infinix Hot 9
Jiandae na Simu Mpya ya Infinix Hot 9 Tarehe 23 Machi 2020 Jiandae na Simu Mpya ya Infinix Hot 9 Tarehe 23 Machi 2020

Baada ya kampuni ya Infinix kuzindua simu mpya ya Infinix S5 Pro zaidi ya siku 10 zilizopita, hivi karibuni tegemea kusikia kuhusu toleo jipya la simu ya Infinix Hot 9 simu ambayo inategemewa kuzinduliwa hivi karibuni.

Kwa mujibu wa akaunti ya Twiiter ya Infinix ya nchini Indonesia, simu hiyo mpya ya Infinix Hot 9 inategemewa kuzinduliwa tarehe 23 mwezi huu huko nchini Indonesia huku simu hiyo ikitarajiwa kuwa na maboresho mengi zaidi.

Advertisement

Jiandae na Simu Mpya ya Infinix Hot 9 Tarehe 23 Machi 2020

Kama inavyo onekana kwenye picha hapo juu, Infinix Hot 9 inaonekana kuja na kamera nne kwa nyuma huku ikiwa na teknolojia ya AI pamoja na Flash ya LED. Pia muundo wa kamera kwenye simu hiyo unaonekana kuwa tofauti na matoleo yaliyopita ya Infinix Hot 8 na Infinix Hot Lite.

Kwa sasa bado hakuna taarifa zaidi kuhusu sifa pamoja na bei ya simu hiyo mpya, kama unataka kujua zaidi kuhusu sifa na muonekano wa simu hii pamoja na taarifa za uzinduzi wa simu hii kwa hapa Tanzania, basi endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku tutakupa habari zaidi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use