Betri yenye ujazo mkubwa kwa matumizi mbalimbali kama vile kucheza games, kuangalia video pasipo hofu ya kuzima ndio mategemeo makubwa tulionayo wadau wa Infinix HOT 10 na hii ni baada ya picha kuvuja kupitia mitandao ya kijamii lakini pia kupitia chanzo cha ndani ya kampuni ya Infinix.
Kwa sisi wadau wa simu za Infinix tunafahamu fika kuwa kampuni ya Infinix inafahamika zaidi duniani kama kampuni ya vijana na wenye kupenda sambambasa na badiliko ya teknolojia lakini pia chanzo cha ndani ya kampuni ya Infinix amedokeza kwa uchache kuhusiana na toleo la Infinix HOT 10 kama ifuatavyo;
Inasemekana Infinix HOT 10 kuwa simu ya kwanza katika toleo la HOT kuja na processor ya MediaTek Helio G70 na teknolojia ya MediaTek Hyper Engine Madhubuti katika uchezaji wa games zenye speed ya juu pasipo kuzidiwa uwezo.
Infinix HOT 10 inasemekana kuwa na kioo kipana cha inch 6.78 chenye kumfaidisha mtumiaji wakati wa kuperuzi mitandaoni na kupata picha halisi pasipo kujali idadi ya watu.
Na kama inavyofamika toleo la HOT ni maalumu kwajili ya vijana wenye kupenda burudani basi inasemekana Infinix HOT 10 ni zaidi ya matoleo ya awali ya HOT kwani HOT 10 huenda ikawa na teknolojia ya DTS Audio kwajili ya kupata mziki mzuri pasipo kutofautisha na waredioni.
Kamera si swala la kuhoji, Infinix imekuwa miongoni mwa makampuni ya simu yenye simu zenye kamera kali, japo haijatambulika HOT 10 kuwa unauwezo gani wa kamera ila inasadikika huenda ikawa na kamera kali zaidi kutokana na picha za mtandaoni kuonyesha kamera 4 nyuma.
Tetesi hizi zinatujuza Infinix kuingia sokoni mapema tarehe 5/10/2020 na itapatikana katika maduka yote ya simu kwa bei nzuri tulizozizoea katika simu za toleo la HOT.