Hivi karibuni kampuni ya Sony ilizindua Simu yake mpya ya Sony Xperia XZ, simu hii ilizinduliwa kwenye tamasha la IFA ambalo lilifanyika huko berlin wiki mbili zilizopita simu hiyo mpya imekuja wakati mwafaka wakati wateja wa Sony wakiwa na kiu ya Simu mpya kutokana na ukimya wa kampuni hiyo.
Hata hivyo kampuni hiyo ya Sony imewekeza kwenye simu hiyo kutokana na simu hiyo kuwa na sifa nzuri pengine kuliko simu zingine za Sony Xperia zilizoko sokoni kwa sasa, simu hiyo mpya inakuja na kamera ya 23MP ikiwa na uwezo mkubwa wa kupiga picha kwenye mwanga hafifu pamoja na simu hiyo inayo uwezo mkubwa wa kuchukua video za 4K kwa kutumia teknolojia ya five-axis stabilization ambayo ina fanana na ile kutoka kwenye Kamera za Sony Handycam cameras. Pia kamera ya mbele ya simu hiyo inayo uwezo wa 13MP ikiwa na teknolojia ya zoom mpaka mara 12.
Ukiacha swala zima la kamera, simu hiyo mpya ya Sony Xperia XL bado ina sifa nyingine nyingi zenye mashiko kama vile muundo wa simu hii ni mzuri sana ukiwa umetengenezwa kwa njia ya (loop surface) pamoja na ubapa wa nyuma wa Aluminum. Pia simu hiyo ya Sony Xperia XL inakuja na kioo cha Inch 5.2 pamoja na teknolojia ya 1080p, kingine zaidi simu hiyo mpya inaendeshwa na processor ya Snapdragon 820 CPU ikiwa na usaidizi wa RAM ya 3GB, vilevile kwenye kuchaji simu hiyo mpya inatumia chaja ya kisasa ya USB Type-C pamoja na uwezo wa kutumia line mbili pamoja na uwezo wa kuongeza memory kwa kutumia memory kadi ya mpaka GB 256.
Kingine kikubwa simu hiyo inakuja na uwezo wa kuzuia maji na vumbi ikiwa na teknolojia ya (IP65/68 water and dust resistance) lakini sony wanatoa tahadhari kuhakikisha kuwa sehemu ya chaji inakauka vizuri kabla ya kuchaji pale simu yako itakapo dumbukia kwenye maji. Kuhusu mfumo wa uendeshaji wa Sony Xperia XL simu hiyo inakuja na Android 6.0 Marshmallow.
Pamoja na hayo yote Sony imeamua kuchukua hatua ya kwanza kuhusu Battery ya simu yake kwa kuweka Programu maalum ambayo inaitwa Battery Care, programu hii itakusaidia kuangalia simu yako pale unapokuwa umeiacha kwenye chaji kwa muda hata baada ya simu hiyo kujaa.
Hata hivyo kwa upande wa simu pacha ya Sony X Compact simu hiyo inakuja na sifa pungufu kidogo kuliko Sony Xperia XL ambayo hii inakuja na kioo cha inch 4.6 pamoja na teknolojia ya 720p, kamera ya 23MP na ya mbele 5MP pamoja na kuendeshwa na processor ya Snapdragon 650 CPU.
Simu hizo zote mbili zinategemewa kuingia sokoni na kuanza kwa mauzo ya awali hapo October 2 mwaka huu. Simu ya Sony Xperia XL inategemewa kuuzwa kuanzia dollar za marekani $699 mpaka dollar $717.59 ambazo ni sawa na shilingi za Tanzania Tsh 1,525,882.05 hadi Tsh 1,566,463.09 hii ni kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya tarehe 25-09-2016.
Ili kufuatili simu hizo zitafika lini hapa Tanzania endelea kutembelea blog ya tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech moja kwa moja kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube kwa kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.