Kampuni ya teknolojia ya nchini china ZTE hivi karibuni imetangaza kuleta simu yake mpya ambayo huna haja ya kuigusa ndio utumie, badala yake simu hii inakupa uwezo wa kuitumia kwa kutumia macho yako.
Simu hiyo iliyopewa jina la Hawkeye imetangazwa kuwa sehemu ya maonyesho kwenye mkutano wa CES wa mwaka huu 2017 utakaofanyika mwezi February. Hata hivyo simu hiyo inatumia kamera ya mbele ili kuangalia uelekeo wa macho yako (iris motion) na kutafsiri uelekeo huo kuwa hatua mbalimbali kama vile kusogeza juu na chini, kusogeza pembeni na hatua nyingine kama hizo.
Kuongezea zaidi ZTE imetangaza kuwa simu hiyo itakuja na kava maalum ambalo litakuwezesha kunatisha simu hiyo kwenye ukuta au sehemu yoyote iliyoko flat, simu hiyo itakuwa na kioo cha inch 5.5 chenye teknolojia ya HD display, vile vile simu hiyo itakuja na teknolojia ya Fingerprint vyote vikiwa vinaendeshwa na Android Nougat 7.0.
Kwa sasa bado ZTE haijasema kuwa simu hiyo itauzwa bei gani, lakini simu hiyo iko kama project kwenye tovuti ya Kickstarter wakati kampuni hiyo ikiomba support kutoka kwa watu mbalimbali ili kukamilisha kiasi cha dollar za marekani $500,000 ili kusaidia kuanza uzalishaji wa simu hiyo.