Moja kati ya swali ambalo tumelipata kupitia kwenye ukurasa wetu wa facebook ni pamoja na hili, ambalo msomaji wetu alikuwa akiuliza “hivi ni kwanini simu yangu imekuwa ikinata nata kila mara au kwa lugha nyingine kwanini simu yangu imekuwa iki staki mara kwa mara hasa app ya instagram”.?
Sasa baada ya uchunguzi na kwa kushirikiana na wataalam mbalimbali wa teknolojia pamoja na watumiaji wa smartphone mbalimbali, zifuatazo ndio sababu za simu yako kustaki kila mara..
Kwenye makala hii tutaweza kuangalia kwanini simu inakuwa na tabia hiyo ikiwa pamoja na njia za kuweza kuepukana na tatizo hilo, basi bila kupoteza muda let’s gooo.
TABLE OF CONTENTS
- 0.1 RAM ya Simu Yako Kuwa Ndogo
- 0.2 Kufungua Progamu Nyingi kwa Wakati Mmoja
- 0.3 Kutumia Programu Zenye Kutumia Internet Kwa Kwasi
- 0.4 Kutumia Programu ya Facebook
- 0.5 Kutumia Programu ya Facebook Messenger
- 0.6 Kutozima Simu kwa Muda Mrefu
- 0.7 Kutofunga Programu baada ya Kumaliza Kutumia
- 0.8 Kutumia Simu Kwa Muda Mrefu ikiwa na Kava
- 1 Mambo ya Kufanya Kuzuia Simu Kuwa Slow au Kustaki
RAM ya Simu Yako Kuwa Ndogo
Moja kati ya sababu kubwa inayofanya simu kuwa na tabia ya kunatanata au kuwa slow ni pamoja na simu kuwa na RAM ndogo. Simu nyingi za bei nafuu huja na uwezo mdogo wa RAM ukilinganisha na programu mtumiaji anazotumia, hii husababisha simu kuwa slow na wakati mwingine kuwa na tabia ya kustaki mara kwa mara.
Kufungua Progamu Nyingi kwa Wakati Mmoja
Kutokana na tatizo la RAM kuwa ndogo, pale unapo fungua programu nyingi kwa wakati mmoja husababisha simu yako kuishiwa na RAM hivyo programu nyingine utakayo ifungua inakosa nafasi kwenye RAM hivyo simu huweza kuwa slow sana au kustaki.
Kutumia Programu Zenye Kutumia Internet Kwa Kwasi
Kama wewe unatumia programu nyingi ambazo zinatuma ujumbe kila mara kama vile WhatsApp, YouTube na pia kama una magroup mengi ya WhatsApp ambayo yanatuma ujumbe kila mara, hii inaweza kuwa sababu ya simu yako kuwa slow au kustaki. Mara nyingi hii husababishwa na programu hizo kutumia RAM kubwa wakati zinatumia internet kuangalia habari mpya ili kukutumia meseji au notification.
Kutumia Programu ya Facebook
Najua Facebook inakuja ikiwa imewekwa ndani ya simu nyingi za Android, lakini kwa mujibu wa utafiti app ya Facebook ni moja kati ya chanzo cha simu kuisha chaji kwa haraka pamoja na kustaki mara kwa mara. Programu hii inachukua karibia MB 200 kwenye simu nyingi za Android na hiyo ni kwa makadirio tu, ukubwa wa programu hii unatofautiana kwenye kila simu.
Kutumia Programu ya Facebook Messenger
Kama ilivyo app ya Facebook pia app ya Facebook Messenger nayo inashutumiwa kutumia RAM kubwa sana, pia app hiyo inashutumiwa kuwa chanzo cha simu kuisha chaji kwa haraka sana. App ya FB Messenger kupitia Play Store inakuja na ukubwa wa MB 47 lakini ukisha install kwenye simu yako app hiyo inatumia karibia MB 200 za ukubwa wa ndani wa simu yako.
Kutozima Simu kwa Muda Mrefu
Kutozima simu kwa muda mrefu ni moja kati ya sababu za simu kuwa slow au kustaki, hii usababishwa na simu kushindwa kufanya baadhi ya vitu kutokana na mrundikano wa programu kwenye RAM ya simu yako. Mara nyingine hata ukifunga programu baada ya kutumia huwa haiondolewi kwenye matumizi ya RAM moja kwa moja hivyo unakuta kuna mlundikano wa programu usizozitumia zikichukua nafasi kwenye RAM ya simu yako.
Kutofunga Programu baada ya Kumaliza Kutumia
Tatizo ambalo hili ni kubwa kwa watu wengi hasa wanaotumia simu za iPhone ni kushindwa kufunga programu baada ya kumaliza kutumia. Hii husababishwa na ile hali ya kubofya kitufe cha kati kati mara baada ya kumaliza kutumia programu badala ya kuifunga kabisa programu yenyewe. Hii husababishwa programu zilizo funguliwa kulimbikizwa na kutumia RAM nyingi na hivyo matokeo yake simu huwa slow au kustaki.
Kutumia Simu Kwa Muda Mrefu ikiwa na Kava
Sababu nyingine ambayo inafanya simu yako kuwa slow au kustaki mara kwa mara ni pamoja na kutumia simu kwa muda mrefu sana huku ikiwa na kava.
Mara nyingi simu za mkononi zime tengenezwa kwaajili ya kutumika kwa muda mfupi, yaani hapa nikiwa na maana kuwa ni mara chache mtu kutumia simu mfululizo kwa masaa bila kupumzika na kama ikitoke hivi basi lazima simu itakuwa slow na itakuwa ya moto sana.
Kwa sababu simu nyingi hazijatengenezwa zikiwa na sehemu za kupooza processor basi kama umefunika simu yako na kava alafu unaitumia kwa muda mrefu ni lazima itakuwa na tatizo hilo na hii ni kutokana na processor ya simu yako kupata joto sana na kushindwa kufanya kazi vizuri.
Mambo ya Kufanya Kuzuia Simu Kuwa Slow au Kustaki
Baada ya kuangalia sababu chache zinazo weza kusababisha simu kuwa slow au kustaki hebu sasa tuangalie njia za kuweza kuzuia simu yako isipatwe na tatizo hili.
- Hakikisha unatumia programu za kuondoa CACHE kwenye simu na epuka programu zenye matangazo mengi. Pia usitumie programu ya Clean Master kwani hii inamatangazo mengi sana na ambayo yanonekana hata kama hutumii programu hiyo.
- Hakikisha unatumia Programu za Facebook Lite na Messenger Lite na ondoa au zima programu ya Facebook ya kawaida.
- Hakikisha unazima simu yako angalu mara nne au tatu kwa wiki hii itasaidia simu yako kudumu na chaji pia itasaidia RAM ya simu yako kuweza kufanya kazi vizuri zaidi.
- Zima Notification kwenye programu ambazo zinatuma ujumbe kila mara, hii itasaidia simu kudumu na chaji pia itasaidia simu kufanya kazi kwa haraka zaidi.
- Hakikisha unafunga programu mara baada ya kumaliza kuitumia na pia hakikisha unazima Internet kwenye simu yako kama huitumii kwa muda huo.
- Kama simu yako inatoka battery hakikisha unazima simu yako na kutoa battery angalau mara moja kwa wiki hii itasaidia sana kuweza kufanya simu yako kufanya kazi haraka. Kama battery yako haitoki basi hakikisha unazima simu yako kwa muda kama dakika 5 angalau mara moja kwa wiki.
- Ni vizuri kama unatumia simu yako kwa muda mrefu utoe kava kwani simu yako itaweza kupoa kwa urahisi kwani kava halitakuwa limezuia sehemu za kupooza simu yako au itasaidia joto la simu kupungua kwa urahisi zaidi.
- Kama App ya Instagram ndio pekee ina tabia ya kustaki mara kwa mara basi hakikisha una Uninstall programu hiyo kisha pakua tena programu hiyo kupitia masoko ya Play Store au App Store.
Na hizo ndio njia chache ambazo unaweza kuzitumia kuweza kufanya simu yako isiwe ina tatizo la kustaki kila mara au kuwa slow.
Kumbuka njia hizi ni baadhi tu ya njia ambazo zinaweza kusaidia kufanya simu yako isiwe na tatizo la kustaki, njia nyingine za kusaidia tatizo hili nategemea kuzipata kutokea kwako kupitia sehemu ya maoni hapo chini..
ticket ya ndege ya fastjet mwanza to dar ni sh ngapi? kwa tarehe 15/09/018
inategemeana na mahali unapo kwenda
nice
Asante sna bro kwa somo zuri ila mm nna swal na nahc n shda nnaweza kupata aaplication za kutrack namba za simu coz kuna mtu kafnya uharfu kaiba hela mtandaon so tunataka tujue alipo
mm simu yangu kwenye snapchat nikichukua video au picha inaenda slow sijui kwanini
Ninapotaka kutumia app Fulani mfano Facebook,istagram, telegram na zingine naambiwa isn’t responding. Mfano unaambiwa telegram au Facebook isn’t responding. Sasa sijui nifanyeje!
Unatakiwa kuhakikisha simu yako ina nafasi ya kutosha, kwa uhakika zaidi hamishia app hizo kwenye memory card.
Asante sana brother kwa somo zuri nimekuelewa vizur.usichoke endelea kutusaidia kwani wengi tunapatwa na shida kama hizi tunashindwa kuzitatua