Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hatimaye Sasa Jiandae na Simu Janja Yenye Kamera Tisa

Fahamu simu inayokuja hivi karibuni yenye kamera au lensi tisa
Smartphone yenye kamera tisa Smartphone yenye kamera tisa

Najua unashangaa baada ya kusoma kichwa cha habari, ni kweli kabisa kama ulikuwa unashangaa simu janja yenye kamera nne sasa itabidi ujiandae na simu janja mpya ambayo inakuja na uwezo wa kamera tisa. Simu janja hiyo inategenezwa na kampuni moja ambayo inaitwa Light, kampuni hii inatabia ya kutengeneza bidhaa za kushangaza kwani mapema mwaka huu kampuni hiyo ilikuja na kamera ya kidigital yenye lensi au kamera kumi na sita (16).

Ndio kamera 16 kwenye kifaa kimoja, Kamera hiyo ya kidigital kwa sasa inapatikana sokoni na inapatikana kwa jina la L16, unaweza kupata kamera hiyo kwa kiasi cha dollar za marekani $2000 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 4,500,000.

Advertisement

Anyway, ukweli hata mimi nimeshangaa kidogo hivyo najua hata wewe utakuwa unataka kujua zaidi kuhusu kamera hiyo, kwa sababu sio mada ya leo kama unataka kujua zaidi kuhusu kamera hii ya L16 unaweza kusoma hapa.

Tukiachana na hayo, hebu tungalie simu janja yenye kamera au lensi 9. Simu hiyo kwa sasa ipo kwenye hatua za majaribio na kwa mujibu wa wataalamu kutoka kampuni ya Light, simu hiyo inauwezo mzuri sana wa kupiga picha hasa wakati wa usiku au kwenye mwanga mdogo, na pia simu janja hii inauwezo wa kupiga picha yenye kiwango cha kamera yenye megapixel 64.

Unaweza kudhani simu hii iko mbali sana kutoka au kuingia sokoni, kama ulikuwa unawaza hivyo basi labda nikwambie, kwa mujibu wa tovuti ya The Washington Post simu janja hii inatarajiwa kuzinduliwa baadae mwaka huu 2018 au mwanzo mwa mwaka ujao 2019.

Kwa sasa kama unataka simu yenye kamera nyingi itakubidi ununue simu ya Huawei P20 Pro ambayo yenyewe inakuja na kamera nne, kamera tatu zikiwa kwa nyuma na kamera moja kwa mbele. Vilevile unaweza kununua simu ya Huawei U12 Plus ambayo yenyewe pia inakuja na kamera nne ambazo mbili ziko kwa nyuma na nyingine mbili ziko kwa mbele.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use