Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Wahandisi Marekani Wabuni Simu ya Mkononi Isiyo Tumia Battery

Sasa jiandae kutumia simu za mkononi zisizo tumia battery
Wahandisi Marekani Wabuni Simu ya Mkononi Isiyo Tumia Battery Wahandisi Marekani Wabuni Simu ya Mkononi Isiyo Tumia Battery

Wengi watu tumekua tukijiuliza kila siku ni kwanini simu za mkononi hazifanyiwi mabadiliko ili kuboresha uwezo wa simu kudumu na chaji kwa muda mrefu.?, kujibu swali hili wataalamu kutoka chuo cha wahandisi Washington wamegundua simu isiyotumia battery.

Wataalamu hao wamefanikiwa kufanya hivyo kwa kutumia teknolojia mpya ambayo inaweza kusaidia simu hiyo kutumia kiasi kidogo sana cha nguvu kuweza kupiga au kupokea simu. Akielezea jinsi simu hiyo inavyofanya kazi professor Paul G. wa chuo cha Allen School of Computer Science & Engineering cha huko marekani alisema kuwa simu hiyo inatumia nguvu ya umeme inayotoka kwenye minara ya redio iliyo karibu (ambient radio signals) na kutumia antenna maalum au ambient light ambazo ndio huingiza umeme wa kiasi cha 3.5 microwatts kwenye simu hiyo ili kuweza kupiga na kupokea simu.

Advertisement

Kwa maelezo zaidi ni kwamba simu hii ina uwezo wa kuchukua nguvu kutoka kwenye signal mbalimbali hivyo kama kuna mahali kuna antenna yoyote ya TV, WiFi au hata mahali popote kwenye radio basi utaweza kutumia simu yako ya mkononi bila kuwa na battery.

Simu hii kwa sasa inakubidi kubonyeza kibonyezo maalum pale unapo ongea na simu na hata pale unapo sikiliza mtu anapo ongea, simu hii inatagemewa kuja kuwa ndio simu za kisasa ambazo zinakuja hapo baadae na inawezekana teknolojia hii ikaondoa matumizi ya simu za mkononi zenye kutumia battery.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use