Wakati kampuni kama Samsung ikiwa bado inaendelea na harakati za kuboresha simu zake zinazo jikunja, kampuni kama LG nayo imeonekana sasa kuanza kufuata nyayo za kampuni ya Samsung kwa kutangaza kuzindua simu yake mpya inayojikunja.
Simu hiyo ambayo hadi sasa inasemekana kupewa jina la Wing, itakua ni simu ya kipekee kutokana na aina yake ya kujikunja kuwa tofauti na simu nyingi ambazo tayari tumesha ziona.
Kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu, kwa mujibu wa tovuti ya the Verge, Wing inategemea kuja na vioo viwili huku kioo kimoja kikijikunja na kufanya simu hiyo kuwa mfano wa herufi T.
Simu hiyo mpya inayotegemewa kuzinduliwa rasmi tarehe 14 mwezi huu, inasemekana kuja na kamera kuu ya Megapixel 64 huku ikitumia processor ya Snapdragon 7-series na simu hiyo ndio itakuwa ya kwanza kutoka kampuni ya LG itakayo kuwa na uwezo huo.
Hata hivyo teknolojia kama hii sio ya kwanza kutumiwa na LG, mwaka jana kampuni ya Samsung ilizindua TV za Sero ambazo nazo zilikuwa zina uwezo wa kuzunguka na kuwa kwenye mtindo wa wa wima kama ilivyokuwa simu hiyo mpya ya Wing kutoka LG.
Kwa sasa bado hakuna taarifa zaidi, kuendelea kujua zaidi kuhusu simu hii mpya ya Wing inayo jikunja kutoka kampuni ya LG, endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.