Kampuni ya Huawei hivi leo inategemea kuja na simu yake mpya ya Huawei Mate 20 pamoja na Huawei Mate 20 Pro. Ingawa bado hatujajua yote kuhusu simu hizi ila ni wazi kuwa simu hizi zitakuwa ni mshindani mkubwa wa simu za Samsung Galaxy Note 9 pamoja na Google Pixel 3 XL kwa upande wa kamera.
Kama nilivyosema ingawa hatujui yote kuhusu simu hizi mpya kutoka Huawei lakini yapo mambo machache ambayo tumefanikiwa kuyajua hivyo kaa nasi hadi mwisho wa makala hii bila shaka na wewe utakuwa unajua haya machache tutakayo kujuza hapa.
Muonekano wa Huawei Mate 20
Kama wewe ni mfuatiliaji wa tovuti ya Tanzania Tach lazima utakuwa unajua kuhusu muonekano wa simu hii mpya ya Huawei Mate 20 na Mate 20 Pro, kama bado wewe ni mgeni hapa basi ngoja ni share nawe muonekano wa simu hii mpya. Kwa mujibu wa mvujishaji maarufu Evan Blass hii ndio picha halisi na muonekano wa Huawei Mate 20.
If you've already seen this — the Mate 20 Pro — I apologize for these five wasted seconds. pic.twitter.com/J18N02hC93
— Evan Blass (@evleaks) October 9, 2018
Kamera za Huawei Mate 20
Kitu kingine ambacho tunakifahamu kuhusu simu mpya za Huawei Mate 20 ni pamoja na kamera, Mwaka huu kampuni ya Huawei imeamua kuja na mfumo wa kamera tatu kwa nyuma kwenye simu zake nyingi za sasa. Ukiangalia Huawei P20 na Huawei P20 Pro zote zinakuja na kamera tatu kwa nyuma pia Huawei Mate 20 na Mate 20 Pro hazina utofauti sana kwani nazo zinakuja na kamera tatu kwa nyuma, Tofauti na kamera tatu kwa nyuma utofauti uliopo kwenye kamera hizi kama unvyo ona kwenye picha hapo juu ni mtindo ambao kamera hizo zimekaa ukiangalia kwa haraka unaweza kusema simu hii inakuja na kamera nne kwa nyuma na sio tatu.
Mengineyo
Mengine ambayo yanatarajiwa kwenye simu hizi mpya za Huawei ni pamoja na fingerprint iliyoko juu ya kioo, pia simu hii inatarajiwa kuja na processor nzuri sana yenye speed kutoka Huawei Kirin 980 pia simu hizi zinategemewa kuja na mfumo wa AI kwenye kamera zake hivyo ni wazi simu hizi zitakuwa zinauwezo mzuri sana kwenye kamera zake. Pia inasemekana kuwa simu hii itakuja na uwezo mkubwa batter ikiwa pamoja na teknolojia mpya ya fast charge.
Na hayo ndio machache yanayotarajiwa kwenye uzinduzi wa simu hizi mpya za Huawei Mate 20 na Mate 20 Pro. Tamasha la uzinduzi wa simu hizi linategemewa kufanyika huko nchini london leo saa kumi kamili (4:00pm) jioni kwa saa za Afrika Mashariki. Kama kawaida Tanzania Tech tutakuwa mubashara kabisa kukuonyesha yote yatakayo jiri kwenye tamasha hilo la uzinduzi wa simu mpya za Huawei Mate 20 hakikisha hupitwi kwa kukaa karibu nasi.